JAPAN YAIPATIA TANZANIA BILL 6.2 KUBORESHA SEKTA YA UVUVI

 

JAPAN YAIPATIA TANZANIA BILL 6.2 KUBORESHA SEKTA YA UVUVI


                                   ***************
Timothy Marko 

Katika kuhakikisha sekta ya kilimo inaimarika SERIKALI ya Japan imeipatia Tanzania msaada washilingi billion 6.2 

Akizungumza na waandishi Habari jijini Dar es salaam Katibu Mkuu wizara ya  Fedha na Mipango Profesa Riziki Shemdoe amesema kuwa fedha hizo zinalenga kuiwezesha shirika lauvuvi la TAFICO kuweza kununua Meli ya uvuvi na mishipi ya ya uvuvi Mita 22 sambamba  na  garila ubaridi lakuhifadhia samaki.

"Miradi mingine nipamoja na ununuzi wa gari la ofisi,ujenzi wa Ghara la ubaridi la kuhifadhi Samaki ununuzi wa mitambo ya kuzalisha  barafu".Alisema Profesa Riziki Shemdoe.

Profesa Shemdoe alisema katika mwaka wafedha 2023/24 Serikali imelenga kulisaidia shiriika hilo katika kuboresha jengo la ghala ubaridi na kujenga ghala lakuhifadhia samaki sambamba na ununuzi naufungaji wamitambo ya kuzalisha barafu. 

Alisema Kutokana uchakafu wa miundombinu serikali katika mwaka wa fedha 2023/24 imelenga kukarabati wa jengo la ghala la ubaridi sambamba naujenzi wa gati la kuegesha meli.

"Ukarabati huu nisehemu  ya maandalizi ya kupokea miradi iliyochini ya Programu ya ESP iliyochini ya ufadhili wa Japani."Aliongeza Profesa Shemdoe  .

Kwa upande wake Muwakilishi wa shirika  la JICA  Hitoshi ARA amesemakuwa Afrika imekuwa ikikabiliwa nachangamoto ya tabiayanchi na usalama wa chakula.

Comments