WAZIRI BITEKO AWATAKA WENYE VIWANDA KUNUNUA MADINI YA WACHIMBAJI WADOGO KWA BEI ELEKEZI
WAZIRI BITEKO AWATAKA WENYE VIWANDA KUNUNUA MADINI YA WACHIMBAJI WADOGO KWA BEI ELEKEZI
Matukio Mbalimbali katika Mkutano wa Wachimbaji Wadogo wa Madini na Wadau wa Madini ya Viwandani.
WAZIRI wa Madini Dkt. Doto Biteko amewataka wadau wa viwanda vya madini kununua madini ya wachimbaji wadogo kwa bei elekezi.
Dkt. Biteko ametoa kauli hiy jijini Dar es Salaam akifungua mkutano wa siku mbili wa wachimbaji wadogo wa madini na wadau wa madini ya viwandani.
Kwamba pamoja na kuwepo kwa bei elekezi wachimbaji wadogo wamekuwa wakilalamika wadau wa viwanda vya madini kuwapunja bei.
“Wenyeviwanda wanatakiwa kununua kwa wachimbaji madini kwa bei elekezi. Pamoja na kuwepo bei elekezi wachimbaji wamekuwa wakilalamika kupunjwa bei.
Wenyeviwanda wanatakiwa kununua kwa wachimbaji madini kwa bei elekezi. Pamoja na kuwepo bei elekezi wachimbaji wamekuwa wakilalamika kupunjwa bei.
Hivyo wenye Viwanda muwasikilize wadau wenu wachimbaji,” amesema Dkt. Biteko.
Waziri Biteko amebainisha kwamba makubaliano ya pamoja ya kuwa na bei elekezi ni ili mwenye kiwanda ajue bei ya kununua madini na mchimbaji ajue bei ya kuuzia.
Hivyo Waziri Biteko amewataka wenye viwanda kuzingatia bei hiyo lengo likiwa ni kuwakomboa wachimbaji wadogo katika umasikini.
Akizungumzia kuhusu mkutano huo ameeleza matumaini yake ni kwamba utasaidia katika kuongeza tija kwenye usimamizi wa sekta hiyo na kuchochea kwenye ukuaji wa pato la taifa.
Ametimia fursa hiyo kuwataka wachimgaji wadogo kuhalikisha madini yao yanakuwa na ubora, kwamba wapo ambao wamekuwa wakichanganya madini yao na vitu vingine ili kuongeza uzito jambo ambalo limekuwa likiwaathiri wenye viwanda.
“Nitoe rai wakati wachimbaji wakilalamika kupunjwa bei nanwenye viwanda na wao wahakikishe wanawauzia madini yenye ubora,” ameongeza Dkt. Biteko.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Dkt. Venance Mwasse amesema kwamba mkutano huo umekutanisha wadau watatu ambao ni wachimbaji wadogo wa madini, wenye viwanda vya madini na taasisi za kifendha.
Dkt. Mwasse amesema wanataka kuhakikisha wachimbaji wadogo wanapata fursa ya kunufaika na rasilimali za nchi.
Katika hatua nyingine STAMICO imetumia mkutano huo kuzindua mpango mkakati wa utoaji wa elimu kwa wachimbaji wadogo wa madini lengo likiwa ni kuwafikia wachimbaji wote nchini.
Kadhalika STAMIKO imesaini makubaliano na makampuni yanayouza vifaa vya uchimbaji wa madini ili kuwawezesha wachimbaji hao wawe wanakodishwa vifaa hivyo kwa gharama nafuu.
Aidha Dkt. Mwasse amesema watasaini mkataba na taasisi za kifedha ili ziweze kuwakopesha mitaji wachimbaji wadogo wa madini.
- Get link
- X
- Other Apps







Comments