Skip to main content

KLINIKI YA UPONYAJI KUANZA LEO NABII S. S ROLINGA NA PROPHET MESERET KUHUDUMIA

 

  KLINIKI YA UPONYAJI KUANZA LEO NABII S. S ROLINGA NA PROPHET MESERET KUHUDUMIA

 


KANISA LA  OMEGA Ministries church of all nation (OCAN) ambayo ipo chini  ya mtoto wa mungu Nabii Samson samwel Rolinga limempokea Nabii Meseret Taye kutoka Ethiopia, Tukio la mapokezi limefanyika Jana Alhamisi 25,Mei 2023 uwanja wa Kimataifa wa ndege Julius Nyerere International airport V. I. P terminal Jijini Dar es Salaam.


Kliniki ya uponyaji ni Kambi maalum ya UPONYAJI kwa muda wa siku tatu mfululizo kuanzia tarehe 26 mpaka 28 Mei 2023 itakayofanyika katika viwanja vya kanisa la omega, mbenzi beach africana Jijini Dar es salaam.Tangu kuanzishwa kwa kliniki ya UPONYAJI mwaka 2019 na huu ni msimu wa tatu hivyo Msimu huu wa Kliniki ya UPONYAJI /HEALING CLINIC mwaka 2023 utaongozwa vizuri na mtoto wa mungu Nabii SS ROLINGA aakiwa na ndugu yake katika kristo Nabii Meseret Taye kutoka Ethiopia.


Nabii SS ROLINGA akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mapokezi ya Nabii Meseret Taye kutoka Ethiopia. 


Kliniki ya UPONYAJI ya msimu huu itakuwa na miujiza  na matendo makuu ya mungu ambayo yanabadilisha historia ya maisha ya watanzania na kizazi chake chote hivyo mtanzania anatakiwa wawalete wagonjwa wa kila aina na wenye shida mbalimbali na watafunguliwa na Yesu kristo. 

Mtoto wa Mungu Nabii SS ROLINGA amesema kuwa siku tatu za kliniki ya UPONYAJI inatoa fursa kwa wagonjwa wa kila aina na wenye shida mbalimbali kupata suluhisho wa matatizo yao kutoka kwa waatalam wa afya na muujiza wa Yesu kristo. 

"Kliniki ya UPONYAJI ni kliniki itakayowajumuisha waatalam mbalimbali wa afya na watoto wa mungu katoa huduma ya kiroho itakayowaponya wagonjwa na watu wenye shida mbalimbali" Alisema SS ROLINGA 

Nabii SS ROLINGA aliongezea na kusema kuwa yeye na Nabii Meseret Taye kwa pamoja ni zao la Nabii TB Joshua. 

Naye Nabii Meseret Taye kutoka Ethiopia amewashukuru OMEGA Ministries church of all nation kwa kuandaa kliniki hiyo muhimu kwa uponyaji kwa wagonjwa na wenye shida mbalimbali. 

PICHA MBALIMBALI ZA TUKIO LA MAPOKEZI YA NABII MESERET TAYE KUTOKA ETHIOPIA UWANJA WA NDEGE JULIUS NYERERE INTERNATIONAL AIRPORT V. I. P TERMINAL 


Comments