MKURUGENZI WA BANDARI DAR, AONGOZA WAFANYAKAZI WA BANDARI HIYO KATIKA MADHIMISHO YA MEI MOSI

 MKURUGENZI WA BANDARI DAR, AONGOZA WAFANYAKAZI WA BANDARI HIYO KATIKA MADHIMISHO YA ME MOSI.

Mkurugenzi wa bandari ya Dar es salaam,Mrisho S Mrisho (aliyekaa katikati)akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa bandari ya Dar es salaam katika sherehe za maadhimisho ya siku Kuu ya wafanyakazi Jana (picha na TPA)
Wafanyakazi wa bandari ya Dar es salaam wakipita mbele ya jukwaa Kuu wakati wa maandamano ya wafanyakazi katika uwanja wa Uhuru wakati wa maadhimisho hayo ya Mei mosi 


NA MWANDISHI WETU. 


Mkurugenzi wa bandari ya Dar es salaam,Bw Mrisho S Mrisho Jana aliungana na wafanyakazi wa bandari hiyo katika kusheherekea sikukuu ya wafanyakazi (mei mosi)ambayo kimkoa sherehe za sikukuu hiyo zimefanyika katika uwanja wa Uhuru Jijini humo na kuhudhuriwa na mkuu wa wilaya ya Temeke aliyemwakilisha mkuu wa Mkoa Amos Makalla. 


Katika maadhimisho hayo yaliyofanyika katika uwanja wa Uhuru, Mkurugenzi huyo wa bandari aliongozana na wafanyakazi wa mamlaka ya bandari Tanzania TPA,bandari ya Dar es salaam katika maandamano yaliyoanzia nje na kumalizika ndani ya uwanja huo wa Uhuru.


Akizungumza na vyombo vya Habari mara baada ya kutamatika Kwa sherehe za maadhimisho hayo Bw Mrisho alisema kuwa bandari ya Dar es salaam itaendelea kuwa kitovu Cha uchumi hapa nchini kutokana na usimamizi madhubuti uliopo Kwa sasa ikiwa ni sambamba na kujali maslahi ya wafanyakazi wa bandari hiyo Kwa kuhakikisha wanaofanya kazi katika mazingira salama. 


Awali Akizungumza katika maadhimisho hayo Kwa niaba ya mkuu wa Mkoa, Mkuu wa wilaya ya Temeke alisema kuwa kama sehemu ya viongozi wataendelea kuhakikisha wafanyakazi wote wa sekta ya umma na binafsi Mkoani humo wanafanya kazi kwenye mazingira wezeshi na yenye staha. 


Comments