TUZO YA MWAJIRI BORA WA MWAKA 2023 KUFAHAMIKA DESEMBA

 

TUZO YA MWAJIRI BORA WA MWAKA 2023 KUFAHAMIKA DESEMBA

                              ********


Waajiri nchini wameombwa kujitokeze kwa wingi kushiriki katika mchakato  wa kumtafuta Mwajiri Bora wa Mwaka ambaye atatangazwa rasmi mapema mwezi Disemba mwaka huu.

Ameyasema hayo leo Mei 30,2023 Mkurugenzi Mkuu wa Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) Suzanne Ndomba wakati wa uzinduzi wa rasmi mchakato wa kutafuta Mwajiri bora wa Mwaka kwa mwaka 2023 uliofanyika katika Ofisi za ATE Jijini Dar es Salaam

Suzanne amewahimiza kwa kuwasihi Wanachama kutembelea tovuti ya tuzo ya Mwaajiri Bora ambayo  itakayowaongoza mpaka kwenye dodoso lililoko mtandaoni.

Aidha amesema  tuzo hizi zimeweza kuchochea na kuongeza tija, mahusiano bora Mahala pa kazi, utii wa sheria na ushindani kibiashara.                                                                                     

Vipengele vya Utoaji wa Tuzo kwa mwaka huu 2023 ni  14 ambavyo ni Ubora katika Usimamizi wa Rasilimali Watu, Tuzo ya Utofautishwaji na Ushirikishwaji

Masuala ya Utawala na Uongozi

Ukuzaji wa Vipaji,Ushirikishwaji wa Mwajiriwa ,wajibikaji katika mwenendo wa biashara na utendaji unaokidhi

Mafunzo ya Ujuzi wa kazi na Uanagenzi ,Maudhui ya Ndani ,Ubora, Uzalishaji na Ubunifu ,Mbadiliko ya Tabia Nchi ,Namna ambavyo makampuni yanakabiliana na Majanga yanayotokea katika Maeneo ya Kazi mfano Janga la UVIKO 19,Usawa wa Kijinsia na Usawa katika Maeneo ya Kazi, ampuni Inayofuata Miongozo na Matakwa ya Kisheria


Comments