ACT WAZALENDO YATAKA MAGARI YOTE YA SERIKALI KUTUMIA NISHATI YA GESI BADALA YA MAFUTA







DAR ES SALAAM

Chama cha ACT WAZALENDO kimeishauri serikali kuanza kutumia nishati ya gesi katika kuendesha magari yote ya serikali ili kupunguza gharama za mafuta ambazo huifanya serikali kutumia gharama kubwa za kuagiza na kununua mafuta hayo.

Hayo yamesemwa na Msemaji wa sekta ya fedha na uchumi wa chama hicho Bi Ester Thomas  wakati chama hicho kikiichambua bajeti ya serikali kwa mwaka 2023/24  iliyosomwa bungeni wiki hii na waziri wa fedha,Mwigulu Nchemba .

Msemaji huyo amesema serikali imekuwa ikitumia gharama kubwa katika kuagiza na kununua mafuta kwa ajili ya magari ya mashirika na taasisi mbalimbali za kiserikali hivyo kama itaanza kutumia nishati ya gesi asilia kwenye magari hayo itaounguza gharama kubwa za uendeshaji na kuzipeleka fedha hizo katika miradi mbalimbali ya maendeleo hapa nchini.

Aidha amesema kuwa  pendekezo la chama hicho kuitaka serikali kutumia nishati ya gesi katika magari yake kupitia gesi asilia [CNG] litapelekea kupunguza matumizi ya serikali kwa takribani shilingi bilioni 500 kwa mwaka,

Hata hivyo kimeshauri bandari zote zaserikali zifugwe mitambo ya kujazia gesi asilia mara moja ili kuanza utekelezaji wa pendekezohilo

Katika hatua nyingine kiongozi mkuu wa chama hicho,Zitto Kabwe amesema kama serikali itaweka kwenye bajeti kwa kutenga fedha nyingi kwa ajili ya huduma za afya kwa wananchi wake ikiwemo upatikanaji wa bima za afya nafuu kwa wannchi hatua hiyo itachochea maendeleo kwani afya bora ndiyo nguzo ya maendeleo

Comments