DCEA YABAINI WANAWAKE KUTUMIKA BIASHARA YA DAWA ZA KULEVYA BILA KUJUA, YAKAMATA MAMIA YA KILO ZA DAWA HIZO.



Na mwandishi wetu,Dar es salaam

Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya (DCEA)imesema imebaini mbinu mpya zinazotumiwa na Wafanyabiashara wa dawa za kulevya ambao huwatumia wanawake katika usambazaji wa dawa hizo bila wao kujua.


Hayo yamesemwa leo June 19,2033 jijini Dar es salaam na kamishna jenerali wa tume hiyo Aretas Lyimo wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya operesheni maalumu ya kukamata na kudhibiti dawa za kulevya iliyofanyika katika mikoa ya Arusha,Dar es salaam,Kilimanjaro na Pwani ambayo imefanikiwa kukamata dawa mbalimbali za kulevya na watuhumiwa wa biashara hiyo.


Kamishna jenerali Lyimo amesema wanawake nchini wanapaswa  kuwa makini pindi wanapotaka kuanzisha mahusiano ya kimapenzi na raia ya wakigeni kwani wamekuwa wakitumiwa na wafanyabiashara wa dawa za kulevya kwa ajili ya usafirishaji wa dawa hizo.



Hatua hiyo imekuja baada ya DCEA kufanya operesheni katika kipindi Cha miezi miwili na wiki tatu ambapo ilibaini  kuwa hiyo mojawapo ya mbinu ambayo  wafanyabiashara wa dawa za kulevya wamekuwa wakiitumia kwa ajili ya kusafirisha dawa za kulevya.


Amesema Wanawake wanapaswa kuwa makini kwani hali hiyo inaweza kuwasababisha kuingia katika matatizo makubwa ya kukamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria huku wanaume wakiwakana.


” Asilimia kubwa ya dawa tulizozikamata tumezikuta zikiwa kwa wanawake una mkuta mtu mmoja anawanawake zaidi ya wawili mpaka watatu na kuficha dawa za kulevya katika makazi yao huku wao wakipanga nyumba tofauti wanakoishi wapenzi wao”amesema Kamshina Jenerali Lymo.

Aliendelea kueleza kuwa hadi sasa jumla ya Wanawake zaidi 20 wamekamatwa na tayari  wapo gerezani kutokana na kukutwa wakiwa wamedhiifadhi dawa hizo ambapo tayari wamefikishwa mahakamani na kesi zao zinaendelea.


” Kifungu cha 15 Cha sheria ya kudhibiti na kupambana na Dawa za kulevya kinaeleza kwamba Ni kosa kusafirisha dawa za kulevya na mtu yoyote atakayethibitika kutenda kosa atawajibishwa kisheria”amesema Kamshina Jenerali Lymo

Aliongeza kuwa Serikali imejipanga ipasavyo kuhakikisha inamaliza tatizo la dawa za kulevya kwa ustawi wa jamii kutokana na kuwepo kwa madhara makubwa ya kiuchumi na kijamii .


Aidha amesema katika Operesheni hiyo  DCEA imefanikiwa kukamata dawa za kulevya aina ya heroin kilogramu 200.5, bagi kavu iliyokuwa tayari kusafirishwa gunia 978, bangi mbichi gunia 5465, bagi iliyosindikwa kilogramu 1.5, methamphetamine gramu 531.43, heroin kete 3878, cocaine kete 138 , mililita 3840 za dawa tiba zenye asili ya kulevya aina ya Pethidine pamoja na kuteketeza ekari 1093 za mashamba ya bangi

Mwisho


Comments