GNM CARGO YAJA NA SAFARI YA KITALII YA KIBIASHARA KWA WATANZANIA CHINA.

 


Katika kuhakikisha watanzania wanapata fursa kibiashara,Kampuni ya GNM Cargo imeandaa safari ya kibiashara na kitalii nchini China ijulikanayo kama “China Business Trip and Fun Walk “ ikilenga kufungua fursa za kibiashara kwa watanzania.


Fursa huyo imetangazwa mbele ya  waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam na Mratibu wa safari hiyo Anthony Luvanda amesema safari hiyo itafanyika mwezi Oktoba kuanzia tarehe 14 hadi 20 mwaka hivyo amewataka Watanzania wanaopenda kuanza au kukuza Biashara zao toka china na hawajui pakuanzia washiriki katika safari hiyo.

Aidha amesema kupitia safari hiyo Watanzania watapata fursa za kibiashara kwa kukutana na watu na kampuni mbalimbali za kichina pamoja na kufungua fursa za utalii kati ya Tanzania na China.

Amesema safari hiyo itahusisha kutembelea maeneo mbalimbali ikiwemo maonyesho makubwa ya kimataifa ya Biashara ya 133 nchini China yajulikanayo kama Canton Fair, viwanda vikubwa vinavyozalisha bidhaa zenye fursa za kibiashara kwa soko la Tanzania na Afrika Mashariki.

Maeneo mengine ni pamoja na viwanda na masoko ambayo yana bidhaa zisizopatikana Tanzania na kujipatia uwakala na eneo la kiutalii la Baiyun Mountain (mlima mweupe).

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Masoko wa GNM Cargo Brigita Mbano amewakaribisha watu kwenye safari hiyo ambayo itafungua fursa mbalimbali za kibiashara na kuhamasisha utalii kwa kuchangia shilingi 6242000 sawa na dola 2550.

Hata hivyo amesema fedha hizo zitajumuisha tiketi ya kwenda na kurudi, huduma za malazi, viingilio katika maeneo ya maonyesho ya Biashara, usafiri ndani ya china kwa maeneo yote watakayotembelea, malipo ya visa na huduma ya mkalimani.

Amesema kwa wale wote watakao nunua bidhaa katika safari hiyo au wakati ujao GNM Cargo inawakaribisha kutumia huduma zake za usafiri kwa gharama nafuu na uhakika.

Comments