RITA YAPOKEA BILIONI 1 KUTOKA ITALY KUBORESHA MFUMO WA USAJILI NCHINI

 

Serikali ya Tanzania imesainiana Mkataba wa Msaada Euro laki nne na elfu kumi sawa na takribani shilingi bilion moja na Serikali ya Italia kwa ajili ya programu ya kuimarisha mfumo wa takwimu na Usajili wa raia ulio chini Taasisi ya Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA ).





Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango wakati wa hafla hiyo Dkt Natu Mwamba amesema lengo za fedha hizo zitakwenda kuwezesha Wakala wa Usajili Ufililisi na Udhamni (RITA) kutekeleza Usajili wa raia na takwimu muhimu kwa ugatuzi wa Usajili wa watoto wenye umri chini ya miaka mitano katika kata 245 na vituo vya afya na hospitali 405 na kufanya JUMLA ya vituo vya kusajili kuwa 650 vyenye isadi ya watoto 348,391 wanaotarajiwa kusajiliwa katika wilaya 11 katika mkoa wa Tanga .


Msaada huu unakwenda kusaidia kitengo cha Usajili,kitengo cha masoko,kitengo cha TEHAMA,kitengo cha Mipango na ufuatiliaji,kitengo cha ununuzi,kitengo cha Usajili ngazi za wilaya katika vitengo hivyo italeta tija kwa watumishi hao wote wafanye kazi kwa ufanisi zaidi na kupunguza watu kukaa foleni kusubiria huduma “amesema Dkt


Hata hivyo Dkt Mwamba amefafanua katika kitengo ikiwemo cha Masoko itasaidia kufanya mikutano kuanzia ngazi za juu kwa maafisa waandamizi,wa mikoa,wilaya,au serikali za mitaa na viongozi wa dini kupitia menejimenti ya RITA na kujenga uelewa wa jamii na kitengo cha TEHAMA fedha hizo zitasaidia vituo vya Usajili vya mikoa na wilaya kufanya majaribio na kusimika mfumo wa uchapaji unaozunguka sehemu hadi sehemu katika mkoa wa Tanga.


Pia katika kitengo cha Ufuatiliaji watumishi wa RITA na serikali za mitaa kufanya utafiti wa awali kwa kukusanya takwimu za awali katika halmashauri lengwa 11 kufanya ufuatiliaji na Usajili tathmini ikihusisha maafisa waandamizi wa mikoa na wilaya timu ya Utawala ya RITA viongozi wa dini na watumishi wahusika na serikali na kitengo cha ununuzi itasaidia ukaguzi wa vifaa

Comments