Skip to main content

CCM DAR ES SALAAM YAJA NA MKUTANO MKUBWA WA HADHARA, KATIBU MKUU CHONGOLO KUHUTUBIA

 

CCM  DAR ES SALAAM YAJA NA MKUTANO MKUBWA WA HADHARA, KATIBU MKUU CHONGOLO KUHUTUBIA



Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mko wa Dar es Salaam Abbas Mtemvu akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

NA MWANDISHI WETU

MWENYEKITI wa Chama cha Maponduzi Mkoa wa Dar es Salaam komendaa mkutano mkubwa wa hadhara utakaofanyika Julai 29, 2023 katika viwanja vya Tanganyika Packers Kawe-Kinondoni.

Hayo yamebainishwa leo Julai 25, 2023 na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Abbas Mtemvu akizungumza na waandishi wa habari.

Mtemvu amesema kwamba lengo la mkutano huo ni kuwaelezea Watanzania kwa kina dhamira ya dhati ya Serikali ya CCM kuwaletea maendeleo.

“Nimelazimika kuzungumza na wakazi wa Dar es Salaam, ikiwa ni katika hatua ya utekelezaji wa maazimio ya kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kilichoketi hivi Karibuni jijini Dodoma,” amesema Mtemvu na kuongeza,

“Kikao kiliazimia Komredi Daniel Godfrey Chongolo Katibu Mkuu wa CCM, kufanya Mikutano Mikubwa ya Hadhara ya kikanda ili kuelezea Watanzania kwa kina dhamira ya dhati ya Serikali ya CCM kuwaletea maendeleo,”.

Hivyo amesema ndiyo maana wameandaa mkutano huo ambao utawapa fursa wananchi wa Dar es Salaam ya kusikia mengi zaidi yaliyofanyika, yanayotarajia kufanyika na yaliyo katika Mikakati na Malengo ya CCM kwa Jiji la Dar es Salaam.

Kwamba mkutano huo utajumuisha burudani za makundi mbalimbali za wasanii na pia utatoa fursa kwa wajasiriamali wadogowadogo kufanya Biashara zao.

Ametoa wito kwa jamaa, Wadau, wakereketwa na wananchi wote Wenye mapenzi mema na CCM kushiriki kwa pamoja kufanikisha nia njema hiyo ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ya kuhakikisha kwa asilimia kubwa wananchi wa Dar es Salaam wanakwenda kusikiliza dhamira ya CCM yakuwaletea Maendeleo.


story na darubiniyahabariblog

Comments