NACHINGWEA WAWAKUMBUKA MASHUJAA WA TANZANIA.

 

NACHINGWEA WAWAKUMBUKA MASHUJAA WA TANZANIA.

 


 Nachingwea.

Leo ikiwa ni kumbukumbu ya Mashujaa waliolipigania taifa la Tanzania kupata Uhuru,ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Nachingwea wameamua kwenda kuwatembelea wagonjwa katika kituo cha afya Cha Naipanga kwa kuwapa zawadi mbalimbali.

Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo akiwa ameambatana na mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea mhandisi Chionda Kawawa wamewatembelea wagonjwa waliolazwa katika kituo cha afya Naipanga.



Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo alisema kuwa wametoa msaada huo kwa ajili kuwakumbuka Mashujaa waliolipigania taifa la Tanzania.

Moyo alisema kuwa kutoa msaada huo kunawakumbusha watanzania kuendelea kukumbukwa Mashujaa waliolipigania taifa la Tanzania na wao kuwa wazalendo wa kweli kwa taifa la Tanzania.



Naye mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea mhandisi Chionda Kawawa alisema kuwa Mashujaa waliolipigania taifa la Tanzania wanatakiwa kuendelea kuwakumbuka kwa kazi kubwa waliyoifanya kuleta Uhuru wa Tanzania na hadi hii leo Tanzania ipo huru

Comments