PAROKO AUAWA KWA KUPIGWA NA ALIYEINGIA KANISANI KWA NGUVU KUTAKA KUSALI
PAROKO AUAWA KWA KUPIGWA NA ALIYEINGIA KANISANI KWA NGUVU KUTAKA KUSALI
Paroko
wa Kanisa la Katoliki, Parokia ya Karatu mkoani Arusha, Pamphili Nada
ameuwa kwa kupigwa na kitu kizito na mtu anayedaiwa kuwa na matatizo ya
afya ya akili aliyeingia Kanisani kwa nguvu kutaka kusali.
Hata
hivyo baada ya mtu huyo aliyejulikana kwa jina la Romani Leonard (30)
kufanya mauaji hayo naye ameuawa na Wananchi wenye hasira.
Kamanda wa polisi mkoa Arusha, Justine Masejo amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo leo Jumatano Julai 19, 2023.
"Padri
alifariki wakati anapelekwa hospitali na mtuhumiwa aliuawa na wananchi
wenye hasira baada ya kupata taarifa za tukio hilo,"amesema.



Comments