TANESCO YAJA NA MPANGO KABAMBE,KULIFIKISHA TAIFA UMEME WA UHAKIKA

Waziri wa Nishati,January Makamba akifurahia jambo akiwa ameambatana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,Albert Chalamila na mkurugenzi mtendaji wa Tanesco Maharage Chance.

 


Mkurugenzi mtendaji wa Tanesco Maharage Chande akizungumza katika Mkutano huo.






Waziri wa Nishati January Makamba akizungumza katika Mkutano huo.

Na Thadei PrayGod

Katika kulifikisha Taifa katika upatikanaji wa uhakika wa Nishati ya umeme hapa nchini SHIRIKA la umemeTanzania (TANESCO) limeezindua ripoti ya mwaka 2021/22 safari ya mabadiliko kuelekea  kuliangaza Taifa, 

Akizungumza katika Mkutano huo leo Julai 31,2023 katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City jijini Dar es salaam ambao pia ulienda sambama na uzinduzi wa mpango mkakati wa shirika hilo kwa kipindi cha miaka 10,Waziri wa Nishati  January Makamba amesema shirika hilo litaendelea kujidhatiti ili kuhakikisha nchi inakuwa na umeme wa uhakika huku akilipongeza shirika hilo katika kusimamia kwake madhubuti mradi wa bwawa la Nyerere ambalo litakapoanza kuzalisha umeme Taifa litapata manufaa makubwa.


Amesema wizara ya Nishati itaendelea kuhakikisha inalisimamia vyema shirika hilo la umeme ili lifikie malengo yake ya kuliangaza Taifa.

"Safari ya mabadiliko ni hatua, bado tunasafari ndefu lakini tutafika, kama wizara tunaahidi kuendelea kuiunga mkono TANESCO ili kuhakikisha inafikia malengo yake, TANESCO ina dhamira kubwa, umeme ni kichecheo kikubwa cha maendeleo ya nchi" 


Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa TANESCO Maharage Chande amesema litaendelea kutoa huduma Bora za umeme hapa nchini kwa kuhakikisha wanaopeleka huduma hiyo maeneo yote hapa nchini.

Amesema hatua iliyofikia mradi wa umeme la bwawa la Mwalimu Nyerere ni ya kuridhisha na utaleta faida kubwa kwa watanzania 

"tutaendelea  kuwekeza zaidi kwenye uzalishaji na usambazaji wa umeme ili wananchi wapate huduma bora, Tunajitahidi kuhakikisha tunatekeleza na kukamilisha mradi wa JNHPP kwa wakati, Mradi wa JNHPP ni muhimu kwa maendeleo ya Taifa na kuhakikisha umeme unakuwa wa kutosha" alisema

 Aidha Chande akieleza kuhusu mafanikio kwa Mwaka wa Fedha 2021/2023, amesema kwamba Shirika limeweza kupata faida ya shilingi biliobi 109.

Kadhalika wameweza kuanzisha namba moja ya huduma kwa wateja, kuunganisha wateja 504,366, kupungua kwa upotevu wa Umeme kutoka asilimia 14.5 hadi asilimia 15 lengo lililowekwa.

Kwamba wanaendelea kuitekeleza Miradi ya kimkakati ukiwemo Mradi wa Mwalimu Julius Nyerere ambao umefikia asilimia 90.

Akizungumzia kuhusu Mpango mkakati wa miaka 10 ijayo, Chande amesema wamejipanga kuwekeza kufanyakazi kidigitali, kuongeza juhudi za kutatua changamoto za wananchi na kuhakikisha kuna mtiririko mzuri wa kifedha.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO Omary Issa ameeleza kuwa Shirika linamkakati mkubwa wa kuandaa Vijana watakao kuja kuliendesha kwa miaka ijayo.

Hivyo amesema kwa sasa kuna kikundi cha watu kiko nje ya Nchi kikipata mafunzo na kwamba hawataishia kwa kikundi hicho tu bali wataendelea na kwa wengine.

Ni wazi kwamba mpango mkakati huo sasa utalifanya shirika hilo kuwa na miradi mikubwa ya umeme na kufanikisha kuliangaza Taifa zima kwa kipindi kifupi.

 


Comments