TANZANIA NA ZANZIBAR ZASAINI HATI YA MAKUBALIANO SEKTA YA MADINI
TANZANIA NA ZANZIBAR ZASAINI HATI YA MAKUBALIANO SEKTA YA MADINI
Waziri
wa Madini Dkt. Doto Biteko ameshuhudia utiaji saini wa Hati ya
Makubaliano kati ya Wizara ya Madini ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania na Wizara ya Maji, Nishati na Madini ya Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar.
Makubaliano
hayo ni mwendelezo wa ushirikiano uliopo baina ya wizara hizo mbili
zilizopo katika upande wa Muungano ikiwa ni maelekezo ya Rais Dkt. Samia
Suluhu Hassan aliyoyatoa Februari, 2023 jijini Arusha ya kushirikiana
kwa lengo la kufanya madini yaliyopo katika maeneo husika yaweza kuleta
manufaa kwa pande zote mbili.
Katika
hafla hiyo iliyofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa ofisi ndogo ya
Wizara ya Madini jijini Dar es Salaam Dkt. Biteko amewataka watendaji wa
wizara hizo kusimamia utekelezaji wa makubaliano
"Maelekezo
ya Mheshimiwa Rais yalitupa dira mpya katika kuendeleza mashirikiano
yetu, hivyo tulichosaini leo sio kwa ajili ya kupiga picha bali ni kwa
ajili ya kazi tuliyojipatia, natamani kuona mambo tuliyosaini hapa
yanakuwa mfano na yanafanyika kwa weledi kwa ajili ya manufaa ya pande
zote mbili," amesema Dkt. Biteko.
Aidha,
Dkt. Biteko amewataka watendaji wakuu wa pande zote mbili kusimamia
masuala hayo ili yaweza kutokea huku akitaka kuanza kusimamia masuala
ambayo hayahitaji rasilimali fedha kubwa ikiwemo kufanya tafiti hivyo
yale yanayowezeka yaanziwe kufanyiwa kazi leo na sio kungoja.
Pia,
amewataka Makatibu Wakuu wa pande zote mbili kutengeneza timu ndogo ya
kusimamia makubaliano hayo ili kuhakikisha ushirikiano huo unadumu na
kuwa wa mafanikio katika pande hizo mbili.
Naye,
Waziri wa Maji, Nishati na Madini Shaibu Hassan amesema utiaji wa saini
wa makubaliano hayo usiishie kwenye makaratasi bali ufanisi na utendaji
unaotakiwa kuonekana ukaonekane.
"Kitendo
kinachofanyika leo ni kitendo muhimu sana kwa kwa pande zote mbili
ambapo viongozi wetu wa juu wamekuwa wakitusisitiza kuendeleza
mashirikiano ambapo tunategemea kushirikiana hasa katika suala la
utaalamu hususan katika kufanya tafiti kwa pamoja," amesema Hassan.
Pia,
Hassan amesema ushirikiano huo utazaa toka kwa pande zote mbili za
muungano na kuwataka watendaji wa wizara yake kufanya kile
kinachowezekana kunyika leo na wasingoje kesho.
Jumla
ya Hati Tano za Makubaliano zimesaniwa kwa taasisi zote zilizo chini ya
wizara ambazo ni Tume ya Madini, Taasisi ya Uwazi na Uwajibikaji katika
Rasilimali Mafuta, Madini na Gesi Asilia, Taasisi ya Jiolojia na
Utafiti wa Madini Tanzania (GST) Shirika la Madini la Taifa (STAMICO)
pamoja na Kituo cha Jemolojia na Tanzania (TGC).








Comments