TCB BENKI KUJENGA MATUNDU YA VYOO 18 SHULE YA MSINGI KIKELELWA ILIYOPO ROMBO MKOANI KILIMANJARO

 

Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kikelelwa wakifurahia matumizi ya majengo yaliyojengwa chini ya ufadhili wa TCB Baada. 

Mkurugenzi wa Hazina akikagua Matundu ya vyoo baada ya kukata utepe akiwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Bi. Chichi Banda. 

Mkurugenzi wa Hazina Bw. Wenceslaus Fungamtama, akikata utepe nawapili kulia ni Afisa elimu idara ya elimu msingi halmashauri ya wilaya ya Rombo Alice Makule na kushoto ni Mwalimu mkuu wa shule hiyo Charles Amos. 
*********

Na Mwandishi wetu

Zaidi ya wanafunzi 700 katika shule ya msingi  Kikelelwa iliyopo wilayani  Rombo mkoani Kilimanjaro wamesaidiwa kuondokana na changamoto ya hatari ya kuambukizana magonjwa mbalimbali ikiwemo kipindupindu hivyo wamepata msaada wa   kujengewa matundu ya vyoo 18 na benki ya Taifa ya biashara (TCB) ambapo hapo awali  walikuwa  wanatumia vyoo  chakavu na  matundu machache.

Akizundua vyoo hivyo shuleni hapo Mkurugenzi wa Hazina Tanzania Commacial  Bank Wenceslaus Fungamtama kwa niaba ya Afisa mtendaji mkuu wa benki hiyo, Sabasaba Moshingi amesema lengo la kujenga vyoo hivyo ni ili kuboresha mazingira na utulivu wa kujifunza kwa wanafunzi hao wawapo shuleni na wasikumbane na changamoto ya magonjwa ya kuambukizana. 

"Ili kuunga jitihada za serikali za kuboresha huduma za kijamii ikiwemo afya na elimu, benki ya TCB hutenga kiasi cha zaidi ya milioni milioni 300 kila mwaka ambapo kwa mwaka huu zimeweza kujenga madarasa, nyumba za walimu na vyoo katika maeneo mbali hapa nchini" amesema Fungamtama.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo Charles Amos ameshukuru benki hiyo kwa kusaidia ujenzi wa matundu ya vyoo kwani mesema  kutokana na uchache wa matundu ya vyoo yaliyokuwepo awali wanafunzi walilazimika kupanga foleni ya kusubiriana huku wale wadogo kujikojolea.

"Tunawatoto waliokuwa wanatoroka kwenda nyumbana kwa aibu ya kujikojolea, hasa muda wa mapumziko ambao wanatoka darasani kwa pamoja, lakini sasa kwa vyoo hivi ni wazi kutakuwa na utulivu wa kujifunza" amefafanua Mwl.Amos

Dada mkuu wa shule  hiyo Careen Jonas ameonyesha furaha yake kuwa licha ya vyoo hivyo kujengwa kisasa, vikizingatia miundombinu ya walemavu lakini pia vina chumba maalumu cha kubadilishia nguo kwa waschana wawapo kwenye siku zao za hedhi. 

Kwa upande wake Afisa elimu idara ya elimu msingi halmashauri ya wilaya ya Rombo Alice Makule, amesema hivi sasa shule inajumla ya wanafunzi 768, wavulana 385 na wasichana 378 ambapo kwa uwiano ilitakiwa kuwe na matundu 16 kwa wavulana na 19 kwa wasichana lakini wakitumia matano matano tu hivyo ujio wa benki hiyo kujenga matundu 18 umepunguza tatizo kwa kiasi kikubwa.

Shule ya msingi Kikelerwa ambayo ipo mpakani mwa Tanzania ni moja kati ya shule kongwe za Mkoa wa Kilimanjaro, licha ya kukabiliwa na changamoto lukuki ikiwemo uchakavu wa madarasa vyoo na uchache wa walimu lakini imeendelea wa kufanya vizuri kitaaluma  kiufaulu.

Comments