WALIMU WATAKIWA KUFUATA MAADILI, MILA NA DESTURI
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi (CCM) Wilaya Kilombero Saidi Mrisho (katikati) akiwa na wajumbe wa kamati ya utekelezaji.
.........................
MWENYEKITI wa Jumuiya ya wazazi Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro Bw Saidi Mrisho amewataka waalumu kuzingatia maadili, Mila na desturi pindi wanapotekeleza majukumu yao ya ufundishaji watoto mashuleni
"Ukuaji wa teknolojia na utandawazi ni jambo lisilokwepeka hivi sasa, lakini walimu mtumike kuwafundisha watoto masuala muhimu bila kuacha kukemea vitendo vibaya kwa watoto ikiwa ni pamoja na ukatili kwa watoto mashuleni"
Mwenyekiti huyo wa Jumuiya ya wazazi akiongozana na kamati ya CCM ameyasema hayo wakati akiongea na waandishi wa Habari kwenye ziara ya kukagua miradi ya maendeleo Wilayani hapo katika kata mbalimbali wilayani hapo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa madarasa kwenye shule za sekondari
Mrisho amesema ifike wakati kila mtumishi wa elimu awajibike kuona elimu inasonga mbele na kuleta matokeo Chanya
Aidha ametoa wito kwa wazazi na walimu kushirikiana katika maelezi ya watoto ili kupunguza mmomonyoko wa maadili na tabia mbaya ambazo zitawaletea matatizo watoto ikiwa ni pamoja na matumizi ya bangi, ubakaji na ulawiti mashuleni
"Nimesikia baadhi ya malalamiko kutoka kwa walimu kutopata ushirikiano kutoka kwa maafisa wa Halmashauri pale wanapopeleka kero, na kuanzia sasa nawataka watumishi wote kuwa kitu Kimoja ili kumsaidia Raisi wetu Dokta Samia Suluhu Hassani katika kuleta maendeleo kwa wananchi" alisema
Nao walimu wametoa shukrani kwa Raisi wa awamu ya Sita kwa mambo makubwa aliyofanya mwaka huu ikiwa ni pamoja na kuwaongeza Mishawaka kimyakimya bila hata kuandikiwa barua, wameshukuru kupatiwa vishkwambi ambavyo vinawasaidia kwa ajili ya mawasiliano kwa kiasi kikubwa kuliko ilivyokuwa hapo awali, lakini pia pesa za madai ya muda mrefu kama vile fedha za uhamisho na madai mengine ambayo yamelipwa kwa wakati na serikali ya awamu ya sita
Kwa upande wawananchi, Subira Omari mkazi wa Tarafa ya Kilombero amepongeza ziara hiyo kwa kuibua kero nyingi pamoja na kuunganisha mawasiliano baina ya wanachama na mashule, na ametoa mfano wa ujenzi wa shule za wazazi na huduma za maji, umeme na chakula kwa wanafunzi
Comments