MWANAHARAKATI AHMED KOMBO AWATAKA VIONGOZI YWA DINI KUTOJIINGIZA KWENYE SIASA AFUNGUKA MAZITO KUHUSU DP WORLD


DAR ES SALAAM

Mwanaaharakati huru hapa nchini Ahmed Kombo amewashauri viongozi wa dini kuacha kuingilia masuala ya kisiasa na badala yake wahubiri dini na kumwacha Rais atekeleze majukumu yake kwa mujibu wa sheria.l

Mwanaharakati huyo ameyasema hayo Jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya masuala mbalimbali ikiwemo suala la uwekezaji wa bandari kati Serikali ya Tanzania na Dubai kupitia DP WORLD.

Aidha mwanaharakati huyo amesema suala la maendeleo siyo suala la mtu binafsi bali  la jamii nzima ndiyo maana Rais Dkt Samia alitafuta wawekezaji kwenye sekta ya bandari ambapo badala yake baadhi ya wanasiasa na viongozi wa dini wameanza kupotosha kuhusu uwekezaji huo kwa kuwahadaa watanzania.

Ameongeza kuwa kwa siku za hivi karibuni amekuwa akipata vitisho kutoka kwa baadhi ya watu Mara baada ya yeye kuamua kukaa upande wa serikali kueleza mema yanayofanywa juu ya uwekezaji hasa wa bandari kwani watu hao wamekuwa wapinga maendeleo na wabinafsi

Hata hivyo Bw Kombo pia amesema Rais asirudi nyuma na apambane kuwaleta wawekezaji na asiyumbishwe na maneno ya watu.

"watanzania tuacheni kufuata mkumbo kwani rais Dkt Samia anapambana kwa ajili yetu tusiyumbishwe na baadhi ya wanasiasa na viongozi wa dini wapinga maendeleo"alisema


Comments