CCM MTAA WA MACHIMBO YAPONGNGEZWA KWA KUTEKEKELEZA ILANI VYEMA
Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi CCM Tawi la Mfuga Ndege Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam imeipongeza Serikali ya Mtaa wa Machimbo kwa kutekeleza Ilani ya chama kwa vitendo.

Hayo yameelezwa na Katibu wa Tawi la Mfuga Ndege Ambrose Mushi wakati alipotembelea Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Machimbo ikiwa ni utekelezaji wa taratibu za chama za kuhakikisha kuwa maelekezo ya Chama, serikali na utatuzi wa changamoto za wananchi zinatekelezwa.
Aidha ameipongeza Serikali ya Mtaa kwa jitihada za kuhakikisha Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Machimbo inakamilika ili mwakani waanze kuitumia kwani kwa sasa wamepanga eneo la kwa ajili ya ofisi.

Ameongeza kuwa katika ziara hiyo pia wanahakikisha kuwa usafi wa mazingira unazingatiwa na taka haziwi kero kwa wananchi kwa kumsimamia mkandarasi kutekeleza wajibu wake wa kuzoa taka.
Kuhusu gharama za uzoaji taka amesema kuwa makubaliano na mkandarasi ni kuwa wananchi watachangia gharama isiyozidi 3000 ambayo hukusanywa na mkandarasi.

Awali akiwasilisha taarifa mbele ya kamati ya Siasa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa machimbo Rahimu Maridadi amesema mambo mengi amefanya ikiwemo ujenzi wa Ofisi ya Serikali ya Mtaa, Kisima cha maji na kuimarisha ulinzi na usalama katika mtaa huo.
Aidha amesema kutokana na ajali za mara kwa mara zinazotokea katika eneo ya Mwisho wa Lami Mkuu wa Wilaya alipotembelea wamekubaliana kuweka vibao vya alama, matuta na eneo ambalo gari huwa zinapata ajali pabaki wazi wafanyabiashara wasifanye biashara eneo hilo.

Aidha amesema wamekubaliana na TANROADS kujenga vizuizi vya nguzo katika eneo hilo lanye mteremko ili ajali inapotokea gari kabla ya kufikia maeneo ya makazi ya watu ikitane na nguzo hizo.
Hata hivyo amesema utekelezaji huo unaanza mara moja na ndani ya wiki ijayo uwe umekamilika isipokuwa utekelezaji wa mda mrefu ni wa kuhamisha kituo cha daladala cha upande wa kushoto kwenda BBuza kurudi nyuma.


Comments