JUMUIYA YA KIISLAMU YAISIHI SERIKALI IWAACHIE MITAALA YA DINI
Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania imeishauri Serikali kuiachia Dini kuandaa Silabasi (Muhtasari) ya Masomo ya Dini ili kulinda imani na itikadi za Dini husika.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Leo August 10/2023 Jijini Dar es salaam Amir Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania Alhajj Sheikh Musa Kundecha Amesema Kwa mujibu wa katiba ya Tanzania Serikali haina Dini.
Ameyasema hayo baada ya kupata taarifa kuwa serikali sasa inasimamia dini na kuifundisha jambo ambalo limewapa mstuko mkubwa.
Aidha ameongeza kuwa hapo mwanzo walikubaliana kuwa Masomo ya dini yataandaliwa na wanadini wenyewe kwa kushirikiana na serikali kuanzia ngazi ya awali hadi vyuo vya ualimu
"Mambo ya Dini yapo nje ya utendaji wa Serikali na kila Dini itasimamia mafunzo ya Dini yake". Amesema Sheikh Kundecha.
Alhaj Sheikh Kundecha ameongeza kuwa katika mkutano wao wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania kilichofanyika Julai 23/2023 waliazimia kumuandikia Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia barua ya kumuomba kukutana nae ili kuangalia jambo hilo.


Comments