Kongamano la Kilimo la World Agrifam lafunguliwa Dar,
Kongamano la Kilimo la World Agrifam lafunguliwa Dar, watanzania watakiwa kushiriki kwa wingi.

WATANZANIA wametakiwa kushiriki kwa wingi katika kongamano la kimataifa la biashara ya mazao ya kilimo World agrifam ili kukuza sekta ya kilimo nchini na kupata masoko ya kuuza bidhaa zao nje ya nchi.

Akizindua kongamano Hilo Jijini Dar es Salaam kwa niaba ya waziri wa biashara Dkt. Ashantu Kijaji Mkurugenzi Mtendaji wa TANTRADE Latifa Khamis amesema ni Jambo la kupongezwa kwa ubalozi wa India kwa kuamua kuleta kongamano hili Nchini Tanzania kwakuwa wakulima wadogo watapata fursa ya kuonana na wahusika wenyewe wanaojihusisha na mazao ya kilimo.
Amesema kwa mazao ya kilimo yamekuwa yakifanya vizuri katika soko la nje hususani zao la parachichi kutoka mbeya hivyo kupitia kongamano hilo watanzania watapata fursa mbalimbali za kukutana na makampuni toka nje kubadilishana uzoefu na masoko ya kuuza mazao yao.
“Hatukutegemea kama zao la parachichi kutoka mbeya lingeweza kufanya vizuri lakini tumeskia namna ambavyo linavyofakazi hivyo ni waombe wakulima wazidi kujitokeza ili kuweza kupata uzoefu wa kilimo”,amesema Latifa .
Hata hivyo Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Pulses Network (TPN) Zirack Andrew ambaye pia ni muandaaji wa kongamano Hilo amesema mkutano huo wa mazao ya chakula unafanyika kwa mara ya kwanza barani Afrika hususan nchini Tanzania
Amesema kongamano hili limefanikiwa kuleta makampuni zaidi ya 700 kutoka nchi mbali mbali duniani kote na ni kongamano ambalo linajumuisha mazao yote yanayolimwa afrika.

Amesema lengo kuu ni kufungua fursa kwa wakulima wa mazao ya jamii ya mikunde korosho mafuta pamoja na pamba kwa kuwa walaji wakubwa wa mazao haya ni bara la Asia ambapi kauli mbiu ya mwaka huu ni “sekta ya chakula Bora kwa ajili ya ustawi wa Afrika”
Amesema tumekuwatanisha wanunuzi kutoka nje na wauzaji wa ndani ili kuweza kubadilishana uzoefu pamoja na uwekezaji katika ongezeko la samani .
“Bado Teknolojia yetu sio nzuri kitu ambacho mazao yetu ya chakula huuzwa chini ya kiwango Hali inayopelekea Bei ya chakula kuwa chini wakati tungeweza kuchakata chakula tungeweza kuuza katika thamani ya juu”amesema Andrew.
Amewataka watanzania ambao bado hawakuweza kufika katika kongamano Hilo ni vyema kufika katika viwanja hivyo vya diamond jublee ili waweze kujifunza vitu mbali mbali.
Amesema kongamano hili limeanza Jana hadi Agost 12 yatahusisha wataalam kutoka nchini India na makundi ya wakulima wa Bara la Afrika.
“Zaidi ya Watu 3000 watatembelea na kushiriki maonesho haya na kampuni zaidi ya 500 zitashiriki, dhamira ni kufungua masoko ya Mazao yetu ya chakula ya Afrika Kimataifa,” amesma Andrew
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Taso Event Organizer Suveer Rajpurohit amesema kwamba wanakuja barani Afrika kwa ajili ya kutafita fursa ya soko kwa mazao ya Kilimo ya Afrika na India.
Amesema kuwa mazingira ya India na Afrika yanafanana kwa kiasi fulani hivyo changamoto zinazokabili sekta ya kilimo zinaweza kutatuliwa kwa pamoja hivyo amewakaribisha wakulima kutembelea maonesho hayo ili kuona fursa mbalimbali zitokanazo na Kilimo.


Comments