MTOTO WA MIAKA 10 AZINDUA KITABU 'FIRST FEMALE PRESIDENT'



Makamo Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Rehema Sombi akiwa ameshika Kitabu cha first female President kilichoandikwa na Mtoto Rafat Simba wakati wa hafla ya uzinduzi wake jijini Dar es Salaam






Makamo mwenyekiti wa UVCCM Taifa Rehema Sombi akiwa ameambatana na baba mzazi wa Mtoto Rafat Simba wakati akiingia ukumbini.



Na PrayGod Thadei,Dar es Salaam

Mtoto Rafat Simba mwenye umri wa miaka kumi amezindua kitababu chake cha kwanza Cha kubuni  kiitwacho 'First Female President'chenye maudhui ya kuwaandaa watoto kuwa watu wakubwa na wenye ushawishi baadaye ambacho pia kimetokana na msukumo na historia ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kama Rais wa kwanza mwanamke Tanzania.


Akizungumza katika uzinduzi wa kitabu hicho uliofanyika katika ukumbi wa Ade Park,Mbezi beach jijini Dar es salaam,Makamo mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi UVCC-Taifa Rehema Sombi amesema kupitia  kitabu hicho siyo tu kimeonyesha ni jinsi gani watoto hasa wa kike wana uwezo wa kufanya mambo makubwa bali kimebeba maudhui makubwa yenye kuwajengea ujasiri watoto na vijana huku akiongeza kuwa sasa umefika wakati kwa wazazi kuwaandaa watoto wao mapema kwa kuwapa elimu na kuwashirikisha katika kazi mbalimbali ikiwemo za nyumbani sambamba na kugundua na kuendeleza vipaji vyao ili kuwajenga kusimama wenyewe wanapokuwa wakubwa na kujenga Taifa bora.

Amesema wazazi wa mtoto huyo wameonyesha uwezo mkubwa kwa jamii kwa kuwajibika na kutimiza sehemu ya ndoto ya binti yao hivyo jamii inapaswa kujifunza kupitia kwao na kitabu cha mtoto huyo kilichozinduliwa.

"Kulea na kutambua vipaji vya  watoto mapema kutasaidia kuwajengea uwezo na kuwaepusha na makundi maovu kwenye jamii  hivyo kitabu hiki nitapeleka nakala yake kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwani kimeonyesha misingi ya utu,umoja na uzalendo"alisema Makamo mwenyekiti huyo

Akizungumza kwa furaha kubwa kwenye uzinduzi wa kitabu chake,mtoto Rafat Simba ambaye ni mwanafunzi wa darasa la sita amesema aliamua kutunga na kuandika kitabu hicho baada ya kuona historia ya Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan pamoja na kushangazwa na kitendo cha Rais kuwa mwanamke jambo lililompa matumaini makubwa kama mtoto wa kike kuamini kuwa wanawake wanaweza kwani hapo mwanzo alikuwa akiamini marais ni wanaume pekee na baadaye aliona maajabu kupitia Rais Mama Samia  "kitabu hichi nilichokizindua leo kitabadilisha mitazamo ya watoto wenzangu wengi hasa wa kike kwa kuamini kuwa mambo yote yanawezekana"alisema


Aidha ameongeza kupitia kitabu hicho,mhusika wake mkuu aliyepewa jina la 'Sakina'atakuwa mfano wa kuigwa kwa watoto wengi kwani kinaelezea jinsi mhusika huyo mkuu katika kitabu hicho alivyopambana mpaka kufikia ndoto zake.
"sikuweza kumaliza masomo yangu ya chekechea kwa sababu walimu wangu waliona uwezo wangu ni mkubwa darasani hivyo nilisoma chekechea kwa miezi mitatu tu na baadaye kuanza darasa la kwanza hata mahafali sikufanya hivyo nitafurahi kuingia darasa la saba mwakani na kufanya mahafali yangu ya kwanza maishani mwangu"aliongeza Rafat

Kwa upande wake baba mzazi wa mtoto huyo Ally Simba amesema yeye kama mzazi amefarijika na ubunifu na kipawa cha mtoto wake na amejitahidi kuhakikisha mtoto anatimiza ndoto zake na kuwa mfano na mwanga kwa watoto wengine wenye ndoto kubwa hapa nchini.
"ni kitendo cha kishujaa kuweka mawazo yako kwenye karatasi na kushiriki mawazo hazo na watu wengine hivyo kitabu hichi ni ushuhuda wa umri wa Rafat hivyo nawaomba watanzania wasome kitabu ili waone maono ya mwandishi huyu mchanga"alisema Bw Simba.

"tuliporudi Tanzania kutokea nchini Rwanda,Rafat aliniambia anataka kugombea nafasi ya uongozi kwenye shule anayosoma na hata nilipomruhusu kushiriki alipigwa chini hakuchaguliwa lakini hakukata tamaa na hatimaye uchaguzi uliofuata aligombea tena na akashinda na sasa ni dada wa shule na hiyo ndiyo maana ya dhana ya kutokata tamaa"aliongeza

Awali akizungumza kabla ya uzinduzi wa kitabu hicho mwanzilishi wa taasisi ya elimu ya mwanga mpya academy,Justine Kakoko ambaye ni mwalimu wa Rafat aliyemjengea uwezo wa kuandika kitabu hicho amesema alianza kumjengea uwezo mtoto Rafat baada ya wazazi wake kugundua kipaji na shauku yake hivyo wakaamua kumpeleka kwake ili ajengewe uwezo wa kitaaluma hali iliyompelekea kuandika kitabu hicho cha First Female President(rais wa kwanza mwanamke).

"Rafat amewekeza vizuri kwenye kusoma vitabu mbalimbali ndiyo maana kawa mwandishi mzuri kwani mwandishi mzuri wa kitabu ni lazima awe msomaji mzuri wa vitabu,kwani pia nilimwambia aje na idea (mawazo}matano na kati ya hayo mawazo matano ya uandishi hili la fist female president lilikuwa zuri zaidi na mwaka mmoja baadaye ya utunzi,uandishi na uandaaji hatimaye leo anazindua kitabu hicho.


Comments