Skip to main content

RAIS DK.MWINYI: SERIKALI ITAENDELEA KUDUMISHA DEMOKRASIA NCHINI

 



NA MWANDISHI WETU

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali itaendelea kudumisha demokrasia nchini  kwa kuyafanyia kazi mapendekezo na michango mbalimbali inayotolewa na vyama vya siasa, viongozi wa dini na asasi za kiraia kwa ustawi wa demokrasia.

Rais Dk.Mwinyi ameyasema hayo leo kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan wakati akifunga Mkutano wa kitaifa wa wadau kujadili hali ya demokrasia nchini kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Vijiji, Mitaa na Vitongoji mwaka 2024 na Uchaguzi Mkuu mwaka 2025 lililofanyika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.

Aidha, Rais Dk.Mwinyi amezindua mradi wa kuimarisha mazungumzo ya vyama vingi vya siasa na kukuza ushirikishi wa Wanawake  na Vijana katika michakato ya kisiasa na chaguzi nchini.

Mkutano huo umeandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) kwa lengo la kujadili hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa maazimio ya Kongamano la kitaifa la Maridhiano, Haki na Amani na kuimarisha mapendekezo ya awali yaliyotolewa na wadau ili kuboresha mazingira ya kisiasa wakati wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi mkuu 2025.

Vilevile, mkutano huo  umehudhuriwa na Wawakilishi wa vyama vya siasa, viongozi  kutoka Serikalini, Mabalozi na wadau wa demokrasia nchini.

Comments