Skip to main content

TASO EVENT ORGANIZER YAJA NA MAONESHO MAKUBWA YA MAZAO YA CHAKULA DAR,KUANZA KESHO

 


Mkurugenzi Mtendaji wa Taso Event Organizer Suveer Rajpurohit akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.


Katika kuhakikisha nchi za bara la Afrika zinashirikiana ipasavyo katika bashara ya chakula na mazao ya chakula na bara la Asia,KAMPUNI ya Taso Event Organizer imeandaa maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Mazao ya Kilimo yatakayofanyika katika ukumbi wa  Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.


Akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 8, 2023 jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Pulses Network,mtandao wa mazao jamii ya mikunde hapa nchini  (TPN) Zirack Andrew amesema mkutano huo wa mazao unafanyika barani Afrika kwa mara ya kwanza katika nchi ya Tanzania ambapo utaenda sambamba na maonesho makubwa ya bidhaa za kilimo ambayo yatakutanisha makampuni zaidi ya 500 ambapo pia zaidi ya watu 3000 wanatarajia kutembdelea maonesho hayo.

Amesema katika mkutano huo ambao utaenda sambamba na maonesho Kutakuwa na vyama mbalimbali vya wakulima na lengo ni kuwakutanisha ili kupata uzoefu na masoko ya Mazao yao,” amesema Andrew na kuongeza,


Amebainisha kwamba zamani Afrika walikuwa wanalima Mazao kwa ajili ya kijikimu, lakini kwa sasa watu wamehama kwenda kilimo cha Biashara, hivyo maonesho haya yatawakutanisha wazalishaji wa Mazao ya chakula wa Afrika na wafanyabiashara wa Kimataifa ambao watayanunua mazoa hayo.

Kwamba kunapokuwepo na siko la uhakika la Mazao kunachochea wakulima kuzalisha zaidi.

Hivyo ametumia fursa hiyo kuwaalika watu wote kuhudhuria maonesho hayo ambapo kutakuwa na mijadala mbalimbali kuhusu Mazao tofauti tofauti, kutakuwa na teknolojia mbalimbali pamoja na kuingia mikataba mbalimbali ya kibiashara.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Taso Event Organizer Suveer Rajpurohit amesema kwamba wanakuja barani Afrika kwa ajili ya kutafita fursa ya soko kwa mazao ya Kilimo ya Afrika na India.

Hivyo amewakaribisha wakulima kutembelea maonesho hayo ili kuona fursa mbalimbali zitokanazo na Kilimo.

Amesema lengo la maonesho na mkutano huo ni kufungua fursa za kibiashara na masoko ya bidhaa za kilimo za Tanzania na Afrika katika bara la Asia.na wanunuzi wa bidhaa hizo kutoka nchi za Asia ikiwemo India ambayo ina idadi kubwa ya watu wanaoweza kumudu bidhaa za chakula kutoka barani Afrika.

Aidha ameongeza kuwa kupitia fursa hiyo wafanyabiasshara ya mazao ya chakula,wakulima watapata fursa ya kukutana 

Kwa upande wake Mbobezi katika Kilimo Biashara kutoka nchini India G. Chandra Shekhar amesema maonesho haya ni muhimu katika kuimarisha na kudumisha mahusiano ya kijamii na kiuchumi baina ya India na Afrika.

Amesema kuwa kupitia maonesho haya, wataweza kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili Kilimo cha Mazao na namna ya kukabiliana nazo ili kuhakikisha Kilimo kinastawi na wakulima wanakua zaidi.

Shekhar amesema kwamba Afrika imekuwa ndiyo mzalishaji Mkuu wa Mazao ya chakula kwa ajili ya Nchi ya India huku India ikiwa ndiyo mzalishaji mkubwa wa Mazao ya Biashara kwa ajili ya Afrika ambapo ametaja baadhi ya Mazao yanayozalisha nchini India na kuletwa Afrika kuwa ni pamoja na Kahawa, Mbegu za mafuta, na mkonge.

Maonesho hayo yanatarajiwa kuanza kufanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee uliopo Upanga jijini Dar es salaam hapo kesho Agost 10 hadi 12,2023 ambapo yatafanyika bila kuwa na kiingilio hivyo watanzania wamehimizwa kuhudhuria maonesho hayo sambamba na mikutano ambayo itafanyika katika ukumbi huo


Comments