BODI YA WAKURUGENZI TAWA YAWAPONGEZA ASKARI WA K9 UNIT JNIA
BODI YA WAKURUGENZI TAWA YAWAPONGEZA ASKARI WA K9 UNIT JNIA.
Dar es salaam,
Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi Mamlaka ya usimamizi ya wanyapori (TAWA) Meja Jenelali (mstaafu) Hamis Semfuko Amewataka Makamanda wa Zone wote Tanzania kuanzisha Vikosi vya Mbwa ili kudhibiti kikamilifu majangili na usafirishaji haramu wa nyara za Serikali.
Ametoa wito huo Umetolewa September 15/2023 jijini Dar Es Salaam wakati wa Ziara ya Bodi ya Wakurugenzi ya TAWA ya kukagua Kazi zinazofanywa na Kikosi cha Mbwa K9 Unit katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl Julias Nyerere (JNIA) ambao wanamafunzo maalumu ya kunusa na kubaini Nyara mbalimbali za Serikali ikiwemo wanyama pori na pembe za ndovu kwa kushirikiana na Askari wanyama pori ikiwa ni pamoja na kutembelea hifadhi ya mbwa mbezi Jogoo, Dar es salaam na kuangalia namna mbwa hao wanavyopata mafunzo.
"Kunatakiwa kuwa na K9 Unit kwenye kila Zone,ambayo itatusaidia kufuatilia Majangili,utoroshaji wa nyara za Serikali na kufuatilia yote yanayotokea katika zone yake" Amesema Semafuko.
Aidha amezitaja changamoto zinazowakabili ikiwemo TAWA katika kutekeleza jukumu la ukaguzi ikiwa na pamoja na Upungufu wa Rasilimali watu na Mbwa"ni changamoto ambazo tunakwenda kuzungumzia kwenye bodi yetu na kutoa uamuzi ambao utahakikisha ya kwamba kazi inafanyika kwa ufanisi katika Airport zote na maeneo yote ya mipaka"
Kadhalika amewapongeza Askari wa TAWA kwa uzalendo,uvumilivu na ukakamavu wao licha ya kuwa wachache wameendelea kufanyakazi saa 24/7 hivyo amewaahidi kwenda kuzitafutia suluhu changamoto zao.
Akizungumza baada ya kuwapokea wajumbe wa bodi ya wakurugenzi TAWA meneja usalama na kaimu mkurugenzi wa Kiwanja cha ndege Lugano Mwansasu amesema kutokana na ukubwa wa maeneo ya ukaguzi wanahitaji idadi ya askari wa wanayapori iongezwe ili kuwe na ufanisi katika ukaguzi.
Amesema kiwanja hicho cha ndege kina sehemu Sita za kazi lakini watendaji ni nane tu Hali ambayo inabidi kufanya kazi kwa mawasiliano pindi linapokea tatizo”
Kwa upande wake Afisa wanyapori Daraja la Kwanza ambaye ni Mkaguzi wa Nyara katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Sayi Mahela Nsabhi, Amesema Kwa kushiriana na Mamlaka na Taasisi mbalimbali, Wamefanikiwa kudhibiti Uturoshaji wa Nyara.“Kikosi kilifanikiwa kudhibiti Utoroshaji wa Nyara wenye jumla ya vipande meno ya tembo 319 vyenye uzito wa kg 250.285, Meno ya simba 20, Kucha za Simba 65, Wadudu hai Nge 638. Na Jumla ya Watuhumiwa 18 Walipatikana katika matukio hayo namashitaka yao yapo katika hatua mbalimbali za Kimahakama Pamoja na kutozwa Faini. Alisema Nsabhi.
Pia Nsabhi ameiomba bodi hiyo kuwapa mafunzo ya mara kwa mara kwa wakaguzi wa nyara za Serikali ili kuweza kuimarisha ufanisi wa utendaji wao kwakuwa watoroshaji wengi wanabuni njia mpya za utoroshaji kwa kubadilisha nyara hizo lakini pia wameiomba bodi kuwa tengenezea na kuwanunulia magari mapya kwani waliyonayo sasa yameharibika.





Comments