JUKATA YAITAKA SERIKALI KUACHANA NA MPANGO WA UTOAJI ELIMU YA KATIBA KWA MIAKA MITATU,YADAI ITACHELEWESHA MCHAKATO
| Mkurugenzi Mkuu wa (JUKATA) Bob Chacha Wangwe |
Na PrayGod Thadei
Siku chache mara baada ya aliyekuwa waziri wa katiba na asaheria
kabla ya kuhamishiwa wizara ya masuala ya kimichezo Dkt Damas Ndumbaro kutoa
taarifa kwa umma juu ya mpango wa serikali kutoa elimu ya katiba kwa miaka
mitatu,Jukwaa la Katiba Tanzania JUKATA limeibuka na kupingana na mpango huo
kwa kudai kuwa utachelewesha mchakato wa katiba mpya
Jukwaa hilo limesema ni vyema Serikali kuanchana na huo wa kutoa Elimu ya
Katiba ya mwaka 1977 na badala yake peleke miswada ya Sheria za michakato wa
katiba Bungeni kwa ajili ya marekebisho.
Akizungumza na Waandishi
wa habari Jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mkuu wa (JUKATA) Bob Chacha Wangwe
amesema ni vyema sasa kwa serikali kuona umuhimu wa kutumia nyaraka muhimu za
mchakato wa katiba Mpya katika kutunga au kurekebisha Sheria za mchakato wa
katiba kwa kuwa zimezingatia mahitaji ya sasa ya nchi pamoja uzoefu wa mchakato
uliokwama mwaka 2014.
Mkurugenzi huyo amesema kuwa kuwa JUKATA mpango huo
uliotangazwa na wizara ya katiba na sheria unapaswa kuangaliwa upya kwani
utasababuisha matumizi mabaya kwa fedha za umma kwani hapo awali mchakato
uluishafanyika kupitia tume ya marekebisho ya sheria.
Hata hivyo Jukwaa hilo limepongeza hatua ya Rais Dkt Samia
kumwondoa katika wizara hiyo Dkt Ndumbaro na kumuweka Dkt Pindi Chana na
limeahidi kufanya naye kazi kwani linaamini uwezo wake katika masuala ya sheria
na katiba.
" Ujio wa Balozi Dkt Pindi Chana katika Wizara ya
Katiba na Sheria tunaamini utaleta nuru ya upatikanaji wa katiba na kuondoa
vikwazo ambavyo kwa namna Moja ama nyingine vitaweza kutukwamisha kama hilo la
kutoa elimu ya Katiba ya mwaka 1977 kwa miaka mitatu " amesema
.
Mwenyekiti
wa Jukata Dkt Ananillea Nkya
Dkt Ananillea Nkya ni mwenyekiti wa Jukata ambaye amesema ni
vyema kwa sasa Mchakato wa upatikanaji katiba mpya kwa kushirikisha na wadau
mbalimbali ili kutengeneza Sheria mfano ambayo itawafanya
watanzania wote wajue namna ya kupata katiba mpya .
‘’niwasihi watanzania wote kuwa kitu kimoja katika kupata
katiba mpya kwakuwa jambo hilo halihitaji kuwa na utashi wa kisiasa hivyo
linahitaji Uzalendo wa maslahi mapana ya kitaifa’’alisema Dkt Nkya
Mjumbe wa bodi ya JUKATA,Deus Kibamba akizungumza na waandishi wa habari
Kwa upande wake Mjumbe wa bodi ya Jukata Deus Kibamba amesema ni vyema sasa kwa waziri wa katiba na sheria Dkt Pindi Chana atoe ratiba ya Mchakato wa katiba mpya ili wadau wote wakae tayari kwa mchakato huo muhimu kwa Taifa na kuongeza kuwa na wao wataendelea kutoa elimu kwa jamii juu ya mchakato wa katiba.


Comments