NDC YATAKIWA KUHARAKISHA MALIPO YA FIDIA KWA WANANCHI,MRADI WA MAKAA YA MAWE NJOMBE


![]() |
| Waziri wa Viwanda na biashara Dkt Ashatu Kijaji Akizungumza katika hafla hiyo. |
Na Thadei PrayGod, Dar es salaam
Uwekezaji ni suala muhimu katika ukuaji wa uchumi imara kwa nchi yoyote duniani.
Uwekezaji huo huleta tija ikiwa pande zote Kati ya serikali na wananchi wamekubaliana kwa pamoja juu ya uwekezaji huo ikiwa ni pamoja na wananchi kulipwa FIDIA ili kupisha mradi huo.
Akizungumza katika hafla fupi jijini Dar es salaam ya utiaji saini mkataba wa mradi wa makaa ya mawe wa Liganga na Mchuchuma uliopo wilayani Ludewa Mkoani Njombe waziri wa Viwanda na Biashara Dkt.Ashatu Kijaji amesema ni vyema kwa Shirika la Maendeleo ya Taifa(NDC),kuharakisha mchakato wa ulipaji fidia kwa wananchi wanaotakiwa kuachia maeneo ili kupisha utekelezaji wa mradi wa mradi huo
Amesema Rais Dkt Samia Suluhu Hassan aliridhia kutoa kiasi cha biilioni 15 .4 za kitanzania kwa ajili ya kuwalipa fidia wananchi wanaotakiwa kuachia maeneo hayo hivyo NDC mpaka kufikia septemba 24 ihakikishe watu wote wamelipwa fidia ili kuanza kwa nomradi huo muhimu kwa umma.

Aidhan Waziri Dkt.Ashatu amewataka wawekezaji hao wazawa waliofanikiwa kusaini mikataba ya uchimbaji madini hayo kuhakikisha wanaaza shughuli za uchimbaji kwa haraka na kufikia kiwango walichokubaliana cha tani 30 kwa mwezi ambapo wawekezaji hao wanamiliki vitalu vitano kwa maana kila mmoja kitalu kimoja.
” Mwekezaji atakayeeshindwa kuaza kuchimba kwa muda tuliokubaliana basi atatupisha ili Serikali impe mwekezaji mwingine kwa maana waliokuwa wameomba kwenye mradi huo walikuwa 25 hivyo wapo stendi bai kwaio jambo la msingi kwenu nikuaza kazi tu,”amesema Waziri huyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mwendeshaji wa NDC Dkt. NIcolaus Shombe,amesema awali mchakato huo ulihusisha jumla ya kampuni 25 kati ya hizo 17 zilifanikiwa kuwasilisha maombi yao kwa ajili ya uchambuzi na ushindani na hatimaye zilipatikana kampuni tano zilizokidhi vigezo .
Alitaja kampuni hizo kuwa ni Sheby Mix investment limited .Nipo Engineering limited .Chusa Mining Company limited .Kindaini Company limited .na Cleveland Mine Service Company limited na mkataba huo utadumu Kwa miaka mitano.
Ameongeza kuwa shirika hilo litaendelea kujidhatiti ili kuhakikisha inalisimamia vyema miradi hiyo ili uwekezaji huo kuleta tija kwa umma.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa kampuni ya Cleveland Mine services Company Ndaisaba Ruhoro alimpongeza Rais Samia kwa kuwaamini wawekezaji wazawa kwa kuamini kuwa wanaweza kulipeleka Taifa katika maendeleo endelevu hivyo watafanya jitihada zote katika uwekezaji huo kwa kutomwangusha Mheshimiwa Raise Dkt Samia na NDC kwa ujumla.
"Imezoeleka katika miradi hii mikubwa kama hiyo wanapewa wageni kutoka nje ya nchi lakini katika kuhakikisha wazawa wanaweza wakikidhi vigezo leo Mheshimiwa Rais kupitia juhudi zake za kukuza sekta ya uwekezaji ametuamini wazawa na wanakwenda kutekeleza mradi huo kama kampuni za kizawa na tunaahidi kuchapa kazi"alisema huku akiiomba serikali kuwaongeza vitalu vingine watakapofanya vizuri katika uchimbaji wa makaa hayo ya mawe ambayo ni rasilimali muhimu duniani.



Comments