TUZO ZA YOUNG CEO ZAZINDULIWA DAR,WAKURUGENZI VIJANA WATAKIWA KUSHIRIKI



Taasisi ya Young CEO imezindua rasmi tuzo maalum za Wakurugenzi vijana Afrika  zinazokwenda kwa jina la ‘ YOUNG CEO s AWARDS 2023’ zinazolenga kutambua mchango , juhudi,nguvu, uwekezaji na ubunifu walioufanya vijana wenye umri chini ya miaka 30 kupitia kampuni zao, taasisi zao, biashara zao au chapa zao.


Tuzo hizo zenye kauli mbiu yake ni ‘TURNING JOB SEEKERS INTO JOB CREATORS’ zitaleta chachu ya maendeleo na ubunifu kwa vijana wengi na kuacha alama yenye ushawishi kwa vijana wengine ikiwa ni pamoja na kubadili fikra za vijana walio wengi katika suala zima la Ajira na Kujiajiri.

Tuzo hizi zimejumuisha sekta 30 tofauti tofauti zitakazokwenda kutoa washindi 30 ambao watatunikiwa tuzo na kutambuliwa na Wadau mbalimbali wa Kitaifa na Kimataifa katika sekta zao husika.

Sambamba na hilo tuzo zimelenga kuibua wakurugenzi vijana vinara katika sekta 30 ikiwemo Teknolojia, Kilimo na Ufugaji, Viwanda , Biashara , Sanaa, Ubunifu na kadhalika.

Dirisha la mapendekezo (Nominations ) limefunguliwa  , mapendekezo hayo yatafanyika kupitia tovuti ya tuzo hizi www.youngceort.or.tz.


Comments