Skip to main content

VIJANA,WAZAZI WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA YA BAJAJI,PIKIPIKI USED KWA BEI NAFUU

 



Wauzaji wa Pikipiki na Bajaji Zilizotumika[used] waliopo eneo la  Keko DDC Jijini Dar es Salaam wametoa wito kwa wazazi na waleze kuwanunulia vijana wao bajaji na pikipiki ili wajiajiri kwani ni salama na zitawasaidia kujikwamua kiuchumi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam Meneja wa wauzaji hao Julius Kato amesema kuwa katika biashara hiyo wameweza kuajiri vijana ambao wanajipatia kipato na wapo pia mikoani ikiwemo Katavi, Mpanda na Shinyanga.

Aidha amewahakikishia watanzania kuwa pikipiki na bajaji hizo ni salama na wanashirikiana na Jeshi la polisi katika kuhakiki usalama wa vyombo hivyo na pale wanapobaini udanganyifu wa taarifa za vyombo hivyo muuzaji hukabidhiwa kwa Jeshi la polisi kwa hatua nyingine za kisheria.

“Tunajua kuwa mkoa wa Dar es Salaam unaongoza kwa wizi wa pikipiki na bajaji hivyo tuko makini sana tukifanya mistake moja jela ipo nje kwa hiyo sisi kujua chombo ni cha halali au sio halali utaalamu huo tunao kujua kadi ni halali au sio na tukigundua sio halali tunapigia polisi wanakuja kumchukua muhusika na kwenda kumalizana nae” Amesema Bw. Kato.

Ameongeza kuwa ili uuze pikipiki na bajaji kwao lazima uwe na taarifa sahihi ikiwemo kadi original yenye jina na kitambulisho picha ndogo na namba ya simu ya muhusika na kujiridhisha zaidi wanampigia muhusika kama kweli anataka kuuza pikipiki au bajaji yake.

Amesema wanauza pikipiki za kuanzia laki nane na kuendelea na mnunuzi wa pikipiki hizo anauwezo wa kutumia kwa kipindi cha miezi 6 na kupata faida akairudisha pikipiki hiyo akaongezea pesa akanunua pikipiki nyingine ya kiwango cha juu zaidi au bajaji.

Hata hivyo amesema pikipiki na bajaji wanazouza wananunua mtaani hususani zile ambazo zinakuwa zimemaliza mkataba wake na kwa wale wenye changamoto wanataka kuuza.

Comments