DULLA MBABE,KATOMPA NGOMA NZITO,KUKIPIGA NOVEMBER JIJINI ARUSHA
Mkurugenzi wa Kampuni ya Lady In Red, Sophia Mwakagenda (Wa pili kulia) ambaye ni mratibu wa pambano la Abdallah Pazi 'Dullah Mbabe' dhidi ya Erick Katompa kutoka Congo (DRC) litakalofanyika jijini Arusha Novemba 25, 2023 akizungumza mbele ya waandishi wa habari hawapo pichani leo Oktoba 23,2023 jijini Dar es Salaam kuhusu maandalizi pambano hilo.
Na Thadei PRAYGODBondia maarufu hapa nchini Abdala Shaban Pazi (Dulla Mbabe) anatarajia kupanda ulingoni kukipiga na bondia kutoka nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo,DRC ERICK Katompa.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam promota Sophia Mwakagenda (Mb)ambaye pia ni mkurugenzi wa kampuni ya Lady in red ambayo ndiyo waandaaji wa pambano hilo amesema pambano hilo limekuja ikiwa ni muda mrefu mabondia hao kupigana chenga.
Amesema pambano hilo linafanyika Novemba 25,2023 jijini Arusha ikiwa pia ni jitihada za kuutangaza utalii hapa nchini kwani wanaamini mapambano ya mchezo wa ngumi yana mchango mkubwa katika kuutangaza utalii wa Taifa.
Aidha amesema pambano hilo kati ya dulla Mbabe na Katompa ambalo litakuwa la raundi 10 litatanguliwa na mapambano mengine (boots) 10 kutoka mabondia mbalimbali ikiwemo wanawake kutoka Arusha.
Kwa upande wake bondia Dulla Mbabe amesema pambano hilo alilisubiri kwa hamu kubwa na atahakikisha anamchapa ipasavyo mpinzani wake.
"hili pambano nilikuwa nalihitaji sana na mwandaaji wa pambano ni wewe mama mkwe kwa hiyo jitahidi sana asije kula kona tena"amesema Dulla Mbabe na kuongeza kuwa,
Anashukuru kwa waandaaji wa pambano hilo kupelekwa Jijini Arusha kwani litautangaza utalii wa Taifa.
ReplyForward |



Comments