KERO YA URASIMISHAJI ARDHI DAR,YAMUIBUA WAZIRI SLAA,ATOA SIKU 7
![]() |
| Waziri wa adhi nyumba na mendeleo ya makazi Jerry SLAA akizungumza na viongozi wa CCM mkoa wa Dares salaam na baadhi ya watendaji wa wizara hiyo. |
![]() |
| Mwenyeiki wa CCM,Mkoa wa Dar es salaam,Abass MTEMVU |
NA THADEI PRAYGOD,DAR ES SALAAM
Kufuatia kuendelea kuwepo kwa baadhi ya changamoto za urasimishaji wa ardhi hususan katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo Jijini Dar es salaam,waziri wa ardhi.nyumba na maendeleo ya makazi,Jerry SLAA ametoa muda wa siku saba kwa naibu katibu mkuu wa wizara hiyo kuzifanyia kazi kero hizo ili wananchi wa mkoa huo wapate hati kwa wakati.
Waziri SLAA ametoa maagizo hayo jijini Dar es salaam wakati Akizungumza na Wataalamu wa Ardhi,
Viongozi wa chama cha Mapinduzi,katika kikao maalum cha kujadili utekelezaji wa ilani ya Chama cha
Mapinduzi kwa upande wa sekta ya ardhi Mkoa wa mkoa huo wenye idadi kubwa zaidi
ya watu hapa nchini.
Aidha waziri huyo amesema
amekuwa akipokea malalamiko juu ya suala la urasimishaji wa ardhi kutoka kwa
wananchi mbalimbali wa mkoa huo hivyo ni wakati sasa kwa naibu katibu mkuu wa
wizara hiyo na watendaji wake kuhakikisha changamoto hiyo wanaifanyia kazi kwa
wakati.
"Natoa maelekezo
yangu kero ya Urasmishaji ni kubwa ,Naibu katibu Mkuu na Watendaji wenzako
tukitoka hapa kwenye kikao mkaanze kushughulikia kero hizi ndani ya siku saba
,mlete taarifa kwa viongozi wa chama,kama kuna tatizo la fedha niambie ili tuone
tunapata wapi fedha ili muweze kukamilisha kazi hii"
Amesema kuwa malalamiko
mengi ya wananchi ni juu ya makampuni ya urasimishaji wa ardhi yaliyopewa
dhamana hiyo kushindwa kuifanya kazi hiyo kwa wakati jambo ambalo limewafanya
wananchi kukosa imani na makampunin hayo na kuacha kuchangia gharama za
urasimishaji,huku akiongeza kuwa serikali imepanga kutoa hati za ardhi milioni
mbili na laki tano mpaka kufikia mwaka 2025.
Hata hivyo katika hatua
nyingine waziri huyo amesema wizara yake inaangalia namna ya kuja na mpango
madhubuti wa kuwa na mikoa maalum ya ardhi katika wilaya zote tano za mkoa wa Dar
es salaam ili kuwafanya wananchi warasimishiwe ardhi zao kwa wakati na hatimaye
kupata hati zao za umiliki.
Abass Mtemvu ni mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM,Mkoa wa Dar es salaam ambaye amsema kero ya urasimishaji ardhi katika mkoa huo imechangiwa kwa kiasi kikubwa pia kutokanana na kuwepo kwa makampuni binafsi ambayo yanachukua fedha za wananchi na kutokomea nazo na kuwaacha wananchi hao wasijue cha kufanya kutokana na makampuni hayo kutofanya kazi ya urasimishaji.





Comments