S3 EDUCATION YAWAKUTANISHA WANAFUNZI,VYUO VIKUU KUTOKA NJE YA NCHI
Na Thadei PrayGod
Taasisi ya masuala ya kielimu ya S 3 Education leo imefanya maonesho ya vyuo vikuu mbalimbali kutoka nje ya Nchi kwa lengo la kutoa fursa kwa wanafunzi hapa nchini kwa ajili ya kujiunga na masomo ya elimu ya juu nje ya nchi.Akizungumza katika mahojiano na Waandishi wa Habari Katika maonesho hayo yaliyonyika katika hoteli ya Serena Jijini Dar es salaam,Meneja wa taasisi hiyo Fatema Salemwalla, amesema kuwa maonesho hayo yatawasadia wanafunzi kupata uelewa mpana wa kozi ambazo wanahitaji kwenda kuzisoma nje ya nchi kwa kukutanisha moja kwa moja na wahusika wa vyuo hivyo.
Bi Salemwalla amesema kuwa Kwenye Maonesho hayo zaidi ya wanafunzi 500 kutoka shule mbalimbali wametembelea na kuweza kukutana fursa mbalimbali za kielimu kutoka katika vyuo vikuu ikiwemo vya nchini Mauritius,UK,Canada,USA,pamoja Ujerumani.
"maonesho haya huwa tunayafanya mara mbili kwa mwaka,lengo ni kutoa fursa kwa vyuo hivi vikuu nje ya nchi kutangaza kozi zao,tunawaalika wanafunzi kupitia shule zao kuja kutembelea maonesho haya,na sasa hivi teknolojia imekuwa kubwa,wanafunzi wanafanya utafiti mapema wa kujua kozi ambazo wanahitaji kusoma kabla hata hawajafika kwenye vyuo husika"amesema Fatema na kuongeza kuwa,
"tupo na idadi ya vyuo vikuu 12 kutoka nje ya nchi ambavyo vimeshiriki Katika maonesho haya na tunahitaji tuendelee kutafuta vyuo vingine zaidi ili kutoa fursa kubwa zaidi kwa wanafunzi wa Kitanzania kutimiza ndoto zao za kielimu kwenda kusoma nje ya nchi"
Kwa upande wao baadhi ya wanafunzi waliotembelea maonesho hayo akiwemo Maryam Suleiman anayesoma kidato cha sita katika shule ya Shaaban Robert Jijini Dar es salaam ambaye amesema kwamba maonesho hayo yatawasadia kama wanafunzi wa Tanzania kutimiza ndoto zao za kusoma nje ya nchi.
"Leo tumepata fursa kubwa ya kutambua vyuo vikuu mbalimbali nje ya nchi ambavyo vina kozi tunazozipenda na wazazi wetu wanao uwezo wa kuvilipia ambavyo vitatupa elimu ambayo itatupa mwanga wa kuja kuwekeza hapa nchini Tanzania"amesema Maryam





Comments