TCRA YATOA ELIMU KWA WADAU WA UTANGAZAJI KANDA YA ZIWA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA
Meneja
wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akizungumza wakati
wa Programu ya utoaji elimu kwa wadau wa utangazaji Kanda ya Ziwa kuhusu
Kanuni Mpya za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta za Kusimamia
Huduma za Utangazaji za Jamii
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mamlaka
ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeendesha Programu ya utoaji elimu kwa
wadau wa utangazaji Kanda ya Ziwa kuhusu Kanuni Mpya za Mawasiliano ya
Kielektroniki na Posta za Kusimamia Huduma za Utangazaji za Jamii ikiwa
ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja.
Mafunzo
hayo yamefanyika leo Alhamisi Oktoba 5,2023 jijini Mwanza ambapo Wadau
wa utangazaji (Redio na watoa huduma za utangazaji kwa njia ya waya).
Katika
Programu hiyo ya utoaji elimu, wadau wa utangazaji wamepewa elimu
kuhusu Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta za kusimamia
Huduma za Utangazaji za Kijamii, Mwongozo kwa watoa huduma za utangazaji
kwa njia ya waya (Guideline for Cable Operators) na Mawasiliano na
TCRA (Tanzanite Portal).
Akifungua
mafunzo hayo, Meneja Kitengo cha Huduma ya Utangazaji kutoka TCRA,
Mhandisi Andrew Kissaka amesema Watangazaji wana nafasi kubwa sana
katika jamii hivyo ni vyema wakafanya kazi kwa weledi kwa kuzingatia
Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta za Kusimamia Huduma za
Utangazaji za Jamii ili kuilinda jamii.
"Jinsi
jamii tunavyoiona inatokana na mambo yanatotolewa kwenye vyombo vya
habari, kama tunafanya vibaya basi pia tunaiharibu jamii, kama
tunatengeneza vipindi vizuri basi tunajenga jamii bora. Mna nafasi kuwa
sana ya kuitengeneza jamii hivyo ni lazima mtengeneze vipindi vya
kujenga jamii ndiyo maana tunatengeneza kanuni za utangazaji ili jamii
iendelee kuwa salama",amesema Mhandisi Kissaka.
"Teknolojia
zinakuja lakini umuhimu wa Redio za kijamii unabaki pale pale hivyo ni
muhimu mtambue kuwa nafasi yenu katika jamii ni kubwa sana",ameongeza Kissaka.
Kwa
upande wake, Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo
amesema wametoa elimu kwa wadau wa utangazaji kuhusu Kanuni Mpya za
Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta za Kusimamia Huduma za Utangazaji
za Jamii ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja.
Mhandisi
Mihayo ametumia fursa hiyo kuwahamasisha watoa huduma za utangazaji
kutumia zaidi mfumo wa kidigitali 'TCRA Tanzanite Portal' kuwa wasiliana
kwa urahisi zaidi na mamlaka hiyo.
"Tunataka
mtumie Digitali zaidi kuwasiliana na TCRA badala ya kutumia muda mwingi
kuja TCRA. Tumieni mfumo wa Tanzanite Portal ili kuokoa gharama na muda
wa kusafiri kufuata huduma, tunataka mtumie digitali kuwasiliana na
TCRA. Ukitaka kuwasiliana na TCRA unaingia kwenye ukurasa wetu unaweka
kile ambacho unataka sisi TCRA tukione",amesema Mhandisi Mihayo.
Katika
hatua nyingine amewataka watangazaji kuzingatia maudhui wanayotoa
kwenye vipindi kwa kuhakikisha wanatumia lugha nzuri ili kujenga jamii
bora.
"Punguzeni
sana kuchanganya lugha, mfano Kiingereza na Kiswahili lakini pia
punguzeni kushabikia mambo ambayo hayako vizuri kwenye vipindi. Epukeni
kushabikia masuala ya kisiasa. Usianze kutangaza kitu ambacho kina
mkwamo kabla ya kuwasiliana na mamlaka husika mfano masuala ya matangazo
ya Waganga wa kienyeji, tiba lishe, nguvu za kiume n.k", amesema Mhandisi Mihayo.
"Mwaka
ujao ni mwaka wa uchaguzi, msishabikie masuala ya kisiasa, msinunulike,
ukialika kiongozi wa chama cha siasa flani hakikisha unaalika na kutoka
chama kingine, ukiona umealika mmoja mwingine hajaja acha hadi wawepo
wote",ameongeza Mihayo.
Meneja
Kitengo cha Huduma ya Utangazaji kutoka TCRA, Mhandisi Andrew Kissaka
akizungumza wakati akifungua Programu ya utoaji elimu kwa wadau wa
utangazaji Kanda ya Ziwa kuhusu Kanuni Mpya za Mawasiliano ya
Kielektroniki na Posta za Kusimamia Huduma za Utangazaji za Jamii. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Meneja
Kitengo cha Huduma ya Utangazaji kutoka TCRA, Mhandisi Andrew Kissaka
akizungumza wakati akifungua Programu ya utoaji elimu kwa wadau wa
utangazaji Kanda ya Ziwa kuhusu Kanuni Mpya za Mawasiliano ya
Kielektroniki na Posta za Kusimamia Huduma za Utangazaji za Jamii
Meneja Kitengo cha Huduma ya Utangazaji kutoka TCRA, Mhandisi Andrew Kissaka akitoa mada kuhusu Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta za kusimamia Huduma za Utangazaji za Kijamii
Meneja
wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akizungumza wakati
wa Programu ya utoaji elimu kwa wadau wa utangazaji Kanda ya Ziwa kuhusu
Kanuni Mpya za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta za Kusimamia
Huduma za Utangazaji za Jamii
Meneja
wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akizungumza wakati
wa Programu ya utoaji elimu kwa wadau wa utangazaji Kanda ya Ziwa kuhusu
Kanuni Mpya za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta za Kusimamia
Huduma za Utangazaji za Jamii
Mhandisi
Mkuu kitengo cha Huduma za Utangazaji TCRA Mhandisi Jan Kaaya
akiwasilisha Mada kuhusu Mwongozo kwa Watoa Huduma za Utangazaji kwa
Njia ya Waya (Guideline For Cable Operators)
Afisa TEHAMA Mkuu TCRA, Irene Kahwili akiwasilisha mada kuhusu Mawasiliano na TCRA (Tanzanite Portal)
Afisa TEHAMA Mkuu TCRA, Irene Kahwili akiwasilisha mada kuhusu Mawasiliano na TCRA (Tanzanite Portal)
Mwenyekiti wa Umoja wa watoa huduma za utangazaji Tanzania (NIBA), Amos Ngosha akizungumza wakati wa mafunzo hayo
Katibu wa Umoja wa watoa huduma za utangazaji Tanzania (NIBA), Heavenlight Kavishe akizungumza wakati wa mafunzo hayo










Comments