TMA YATANGAZA UWEPO WA MVUA ZA EL-NINO,YATOA TAHADHARI HII
Hali ya joto la Bahari katika eneo la kati la kitropiki la bahari ya Pasifiki linatarajiwa
kuendelea kuwa la juu ya wastani katika kipindi cha Novemba, 2023 hadi Aprili, 2024. Hali
hii inaashiria kuendelea kuwepo kwa hali ya El-Niño. Hata hivyo, hali ya El-Niño inatarajiwa
kupungua nguvu kadiri tunavyoelekea mwisho wa msimu wa mvua. Kwa upande wa Bahari
ya Hindi, hali ya joto la bahari la juu ya wastani inatarajiwa kuendelea kuwepo upande wa
magharibi mwa bahari kwa msimu wote wa mvua za Novemba, 2023 hadi Aprili, 2024. Hali
kadhalika joto la bahari la chini ya wastani hadi wastani linatarajiwa kuendelea kuwepo kwa
upande wa mashariki mwa Bahari ya Hindi, hususan katika kipindi cha nusu ya kwanza ya
msimu. Hali hii inaashiria kuendelea kuwepo kwa hali inayotambulika kama “Positive Indian
Ocean Dipole (IOD)” katika nusu ya kwanza ya msimu wa mvua na baadae kupungua
nguvu katika nusu ya pili ya msimu (Februari hadi Aprili, 2024). Kwa upande wa Bahari ya
Atlantiki, joto la bahari la wastani hadi Juu kidogo ya wastani linatarajiwa kuwepo katika
eneo la mashariki mwa bahari.
Kwa ujumla hali hii inatarajiwa kuimarisha mifumo inayosababisha mvua nchini hasa kipindi
cha nusu ya kwanza ya msimu.
Kwa upande mwingine, upepo kutoka misitu ya Kongo kuelekea nchini unatarajiwa
kuimarika hasa katika nusu ya kwanza ya msimu. Hali hii inatarajiwa kuimarisha makutano
ya upepo katika maeneo ya kati na mashariki mwa nchi, hali itakayochangia kuimarisha
mifumo isababishayo mvua nchini.
3. ATHARI NA USHAURI
Athari na ushauri umeandaliwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa kwa kushirikiana na wataalam
wa sekta husika katika mkutano wa wadau wa hali ya hewa uliofanyika tarehe 27
Oktoba, 2023.
a) Kilimo na Usalama wa Chakula
Vipindi vya unyevu wa kuzidi kiasi pamoja na mafuriko vinaweza kujitokeza na kuathiri
ukuaji wa mazao na miundombinu ya kilimo. Magonjwa kama vile ukungu (Fungus)
yanatajariwa kuongezeka na kuathiri mazao kama viazi mviringo, nyanya, ufuta na
maharage. Hata hivyo, shughuli za kilimo zinatarajiwa kuendelea kama ilivyo kawaida
hususan katika maeneo yanayotarajiwa kupata mvua za Wastani hadi Juu ya Wastani
Wakulima wanashauriwa kuandaa mashamba, kupanda, kupalilia na kutumia pembejeo
husika kwa wakati, kutumia mbinu bora na teknolojia za kuzuia maji kutuama shambani,
mmomonyoko na upotevu wa rutuba, na kuchagua mbegu na mazao sahihi kwa ajili ya
msimu huu. Aidha, inashauriwa kuimarisha miundombinu ya kilimo pamoja na uvunaji
maji ya mvua na kudhibiti visumbufu vya mimea ili kupunguza athari zinazoweza
kujitokeza.
b) Mifugo na Uvuvi
Wafugaji na wavuvi wanatarajiwa kufaidika na upatikanaji wa malisho, maji na chakula
cha samaki. Hata hivyo, milipuko ya magonjwa ya mifugo kama vile ugonjwa wa homa ya
Mawasiliano yote yaelekezwe kwa:
Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, Chuo Kikuu cha Dodoma,
Jengo la Utawala, Ndaki ya Sayansi za Kompyuta na Elimu Angavu, 1 Mtaa wa CIVE,
S.L.P 27, 41218 Dodoma; Simu: +255 26 2962610: Nukushi: +255 26 2962610
Barua pepe; met@meteo.go.tz; Tovuti: www.meteo.go.tz
(IMETHIBITISHWA – ISO 9001:2015, Huduma za Hali ya Hewa kwa Usafiri wa Anga)
Page 6 of 10 727K – 03/2023
bonde la ufa, midomo na kwato, na kuzaliana kwa wadudu wanaosambaza magojwa
inaweza kujitokeza. Vilevile, matukio ya kuongezeka kwa magonjwa ya mwani baharini na
kupungua kwa uzalishaji wa mwani kutokana na kupungua kwa kiwango cha chumvi ya
maji ya bahari vinatarajiwa. Aidha, uharibifu wa mabwawa ya samaki kutokana na
ongezeko la mvua unaweza kujitokeza.
Wafugaji wanashauriwa kutumia mbinu bora za ufugaji ili kutunza malisho na kuvuna maji
ya mvua kwa matumizi ya baadae. Jamii inashauriwa kuweka mipango mizuri ya
matumizi bora ya maji na malisho. Wakulima wa mwani wanashauriwa kulima mwani
kwenye maji ya kina kirefu ili kuondokana na athari za maji ya mvua yanayokuwa
yanaingia baharini. Aidha, Wafugaji na wavuvi wanashauriwa kufuatilia mirejeo ya tabiri
za hali ya hewa na ushauri kutoka kwa maafisa ugani ili kupunguza athari zinazoweza
kujitokeza na kuongeza tija katika msimu huu wa mvua.
c) Utalii na Wanyamapori
Hali ya malisho na maji kwa ajili ya wanyamapori katika mbuga na hifadhi inatarajiwa
kuwa nzuri. Hata hivyo, wingi wa mvua unaotarajiwa katika maeneo mengi unaweza
kusababisha kutuama na kusambaa kwa maji na kupelekea wanyamapori kuhama,
hususan katika maeneo yanayotarajiwa kupata mvua za Juu ya Wastani hadi Wastani.
Hali hii inaweza kusababisha magonjwa ya wanyamapori kusambaa kwa wanyama
wanaofugwa na binadamu kutokana na wanyamapori kuingia katika makazi ya jamii
zinazozunguka hifadhi na mbuga. Pia, hali hii inaweza kusababisha hatari kwa binadamu
na wanyama wanaofugwa kutokana na kushambuliwa na wanyama wakali.
Mamlaka husika zinashauriwa kuboresha miundombinu mbalimbali katika hifadhi za
wanyamapori na kujenga uelewa kwa jamii ili kupunguza athari zinazoweza kujitokeza
kutokana na hali ya mvua inayotarajiwa. Hivyo basi, jamii inashauriwa kutoa taarifa kwa
mamlaka husika iwapo wanyamapori wataingia katika makazi au maeneo mbalimbali ya
watu.
d) Usafiri na Usafirishaji
Kutokana na utabiri huu, miundombinu ya usafiri na usafirishaji inaweza kuathirika
hususan maeneo yanayotarajiwa kupata mvua za Juu ya Wastani. Matukio ya hali mbaya
ya hewa yanaweza kuharibu miundombinu ya barabara na reli, ongezeko la ajali
barabarani katika usafiri wa nchi kavu (barabara na reli); kuchelewa au kusitishwa kwa
safari za ndege na reli; mawasiliano hafifu angani na majini; na kuongezeka kwa gharama
za uendeshaji katika shughuli za usafiri na usafirishaji kwa ujumla. Wadau wa sekta hii
wanashauriwa kuchukua hatua stahiki katika utekelezaji wa ujenzi wa miundombinu
mbalimbali pamoja na ukaguzi wa mara kwa mara wa miundombinu ya usafiri na
usafirishaji ili kupunguza athari zinazoweza kujitokeza.
e) Nishati, Maji na Madini
Upatikanaji wa maji unatarajiwa kuimarika, hususan katika maeneo yanayotarajiwa kupata
mvua za Wastani na Juu ya Wastani. Kina cha maji katika mabwawa, maziwa na mito
kinatarajiwa kuongezeka. Hivyo, athari katika miundombinu ya rasilimali maji, usambazaji
Mawasiliano yote yaelekezwe kwa:
Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, Chuo Kikuu cha Dodoma,
Jengo la Utawala, Ndaki ya Sayansi za Kompyuta na Elimu Angavu, 1 Mtaa wa CIVE,
S.L.P 27, 41218 Dodoma; Simu: +255 26 2962610: Nukushi: +255 26 2962610
Barua pepe; met@meteo.go.tz; Tovuti: www.meteo.go.tz
(IMETHIBITISHWA – ISO 9001:2015, Huduma za Hali ya Hewa kwa Usafiri wa Anga)
Page 7 of 10 727K – 03/2023
maji, uchimbaji mdogo wa madini na nishati inaweza kujitokeza. Shughuli za uchimbaji
madini hususan katika migodi midogo zifanyike kwa kuzingatia tahadhari zinazotolewa
kwani ongezeko la maji katika udongo linaweza kusababisha maporomoko ya ardhi.
Wadau wanashauriwa kuzingatia matumizi endelevu na uhifadhi wa rasilimali maji katika
shughuli za uchakataji wa madini, uzalishaji wa umeme, matumizi ya viwandani na
majumbani. Hali kadhalika, mamlaka husika zinashauriwa kuimarisha miundombinu ya
rasimali za maji na kuweka mipango madhubuti ya uzalishaji wa nishati ya umeme kutoka
vyanzo mbadala kama vile nishati ya jua, jotoardhi, upepo na gesi endapo kutatokea
uharibifu wa miundombinu kutokana na athari za mvua za Juu ya Wastani.
f) Mamlaka za Miji na Wilaya
Vipindi vya mvua kubwa vinaweza kusababisha kutuama kwa maji na mafuriko. Hali hii
inaweza kusababisha uharibifu wa miundombinu na upotevu wa maisha na mali. Mamlaka
za Miji na Wilaya zinashauriwa kuboresha mifumo ya mifereji ya maji ili kupunguza athari
zinazoweza kusababishwa na mafuriko sambamba na kutoa elimu kwa jamii juu ya hatua
zinazopaswa kuchukuliwa. Hatua hizo ni pamoja na kuimarisha Kamati za Usimamizi wa
Maafa ngazi za kijiji na Wilaya ili ziweze kujiandaa, kukabiliana na kupunguza athari pindi
zitakapotokea.
g) Sekta ya Afya
Magonjwa ya mlipuko yanaweza kujitokeza kutokana na uharibifu wa miundombinu ya maji
taka unaoweza kusababishwa na maji kutuama na kutiririka. Hivyo, jamii inashauriwa
kuchukua hatua kuhakikisha usafi wa mazingira yanayowazunguka, kuharibu mazalia ya
mbu na kudumisha usafi kwa ujumla. Mamlaka za afya zinashauriwa kuchukua hatua
stahiki kupunguza athari zinazoweza kujitokeza, ikiwa ni pamoja na kuhimiza wananchi
kutibu maji kabla ya kutumia, pamoja na kunywa maji safi na salama. Pia, kuhakikisha
uwepo wa dawa za kutosha katika vituo vya afya kwa kuzingatia uwezekano wa uharibifu
wa miundombinu ya usafirishaji.
h) Sekta Binafsi
Shughuli za kilimo na uzalishaji viwandani zinatarajiwa kunufaika kutokana na mvua za
kutosha zinazotarajiwa katika msimu huu. Hata hivyo, wingi wa mvua unaweza kupelekea
athari katika shughuli za ujenzi wa miundombinu, uhifadhi na usafirishaji wa mazao tete
na bidhaa.
Wadau wa Sekta Binafsi wanashauriwa kushirikiana na wataalamu mbalimbali ikiwemo
wataalam wa hali ya hewa ili kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza. Taasisi za
Benki na Bima zinashauriwa kuandaa na kutoa huduma mahususi kwa wadau ili kujenga
ustahimilivu katika biashara.
i) Menejimenti za Maafa
Mawasiliano yote yaelekezwe kwa:
Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, Chuo Kikuu cha Dodoma,
Jengo la Utawala, Ndaki ya Sayansi za Kompyuta na Elimu Angavu, 1 Mtaa wa CIVE,
S.L.P 27, 41218 Dodoma; Simu: +255 26 2962610: Nukushi: +255 26 2962610
Barua pepe; met@meteo.go.tz; Tovuti: www.meteo.go.tz
(IMETHIBITISHWA – ISO 9001:2015, Huduma za Hali ya Hewa kwa Usafiri wa Anga)
Page 8 of 10 727K – 03/2023
Katika maeneo yanayotarajiwa kupata mvua za Juu ya Wastani hadi Wastani vipindi vya
mvua kubwa vinaweza kujitokeza na kusababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi na
kupelekea uharibifu wa miundombinu, mazingira, upotevu wa mali na madhara kwa
binadamu. Hivyo, Idara ya Menejimenti ya Maafa nchini inashauriwa kuendelea kuratibu
utekelezaji wa mipango itakayosaidia kupunguza madhara yanayoweza kujitokeza. Aidha,
sekta, mamlaka husika na Kamati za Usimamizi wa Maafa katika ngazi ya Mkoa, Wilaya,
Kata na Vijiji/Mitaa zinashauriwa kuchukua hatua stahiki ikiwemo kutoa elimu na miongozo
itakayohamasisha kuzuia au kupunguza madhara.
j) Vyombo vya Habari
Vyombo vya habari vinashauriwa kupata utabiri, kufuatilia na kusambaza taarifa na
tahadhari za hali ya hewa pamoja na zile zilizo huishwa na Mamlaka. Vyombo vya habari
pia vinashauriwa kutafuta na kutumia ushauri wa kisekta kutoka sekta husika wakati wa
kuandaa na kutoa taarifa mtambuka za hali ya hewa kwa jamii. Aidha, vyombo vya habari
vinashauriwa kuandaa na kusambaza makala za kitaalamu kwa kutumia lugha nyepesi kwa
lengo la kuhabarisha jamii juu ya matumizi sahihi ya utabiri wa hali ya hewa. Vilevile,
kushirikiana na wataalam wa sekta husika katika kuandaa vipindi maalum vya kutoa elimu
na kwa wakati kuhusu athari mbalimbali za hali ya hewa zinazotarajiwa kutokea na hatua
zinazopaswa kuchukuliwa ili kukabiliana na athari hizo.
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania inawashauri watumiaji wa taarifa za hali ya hewa ikiwa
ni pamoja na wakulima, wafugaji, Mamlaka za Wanyamapori, Mamlaka za Maji na Afya
waendelee kutafuta, kupata na kuzingatia ushauri wa wataalamu katika sekta husika.
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania itaendelea kufuatilia mwenendo wa mifumo ya hali ya
hewa na kutoa mirejesho ya mwelekeo wa mvua nchini kadri inavyohitajika. Aidha, wadau
wanashauriwa kuwasiliana na Mamlaka ili kupata taarifa mahsusi za utabiri wa msimu ili
kukidhi mahitaji maalum katika sekta zao.
Imetolewa: 31 Oktoba, 2023
Na: Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania
Comments