MIAKA 62 YA UHURU ,RAIS SAMIA KUZINDUA DIRA YA MAENDELEO,KUTOA UJUMBE MAALUM
Waziri
wa nchi ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Kitila Mkumbo akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Desemba Mosi, 2023
wakati wa kutambulisha rasmi siku ya uzinduzi wa Dira ya Maendeleo ya
Kitaifa utakaofanyika Decemba 9, 2023.
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Lawrence Mafuru akifafanua
jambo kwa waandishi wa habari jjini Dar es Salaam leo Desemba Mosi,
2023.
Na mwandishi wetu,
RAIS
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan
anatarajiwa kufungua mkutano wa kwanza wa kitaifa wa Dira ya Maendeleo
ya Kitaifa utakaofanyika Decemba 9, 2023 katika kituo cha Kimataifa cha
Mikutano Cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Wakati
huo huo Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kutumia siku hiyo
kutoa ujumbe maalumu wa kuadhimisha miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania Bara
na kuzindua timu kuu ya kitaalamu ya dira pamoja na nyenzo za kidijitali
zitakazotumika katika kukusanya maoni ya wadau.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Desemba Mosi, 2023,
Waziri wa nchi ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Kitila Mkumbo
amesema kuwa lengo mkutano huo litakuwa ni Kuzindua, Kupokea na kujadili
taarifa ya Kitafiti ya tathmini ya utekelezaji wa Dira ya Taifa ya
Maendeleo ya 2025.
Amesema
taarifa ya kitafiti ya tathmini ya Utekelezaji wa Dira ya Taifa ya
Maendeleo ya 2025, imeainisha mafanikio yaliyopatikana na changamoto
zilizojitokeza katika utekelezaji wa dira ya taifa ya kwanza ya Taifa ya
Maendeleo ambayo ilianza kutekelezwa mwaka 2000 na itafikia mwisho
2025.
Ameeleza
kuwa taarifa ya tathmini itaonesha pato la mtanzania ambalo
limeongezeka kutoka dola za kimarekani 399.5 ambazo ni shilingi
322,597,000/# kwa mwaka 2000 hafi kufikia dola za Marekani 1200 ambazo
ni shilingi 2,880,000/# kwa mwaka 2022.
Pia
taarifa hiyo itaonesha utoshelevu wa Chakula kwa asilimia 124
ikilinganishwa na lengo la kufikia asilimia 140 ifikapo 2025, hatua hiyo
imewezesha Tanzania kukabiliana na njaa kwa mikoa na wilaya zote
nchini.
Mtandao
wa barabara za lami na zege katika mikoa umeongezeka kutoka kilomota
4,179 kwa mwaka 2000 hadi kufikia kilomita 11,966.38 kwa mwaka 2023.
Mafanikio
mengine ni pamoja na kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi kutoka vifo
760 kwa vizazi hai 100,000 kwa mwaka 2000 hadi kufikia vifo 104 kwa
mwaka 2022 ikiwa lengo limevukwa la kufikia vifo 260 ifikapo 2025.
Pia
amesema wadau mbalimbali 971 watahudhuria mkutano huo ikiwa pamoja na
viongozi wakuu wa SerIkali ya Muungano wa vyama vya siasa, viongozi wa
taasisi za dini viongozi wa taasisi mbalimbali na za sekta binafsi,
viongozi wa makundi mbalimbali ya kijamii, yakiwemo wazee, watu wenye
ulemavu, wakulima, wafugaji, wavuvi na wachimbaji madini, jumuiya za
kimataifa, wasomi waandishi wa habari.
Wananchi
wameombwa na kusisitizwa kufuatilia mchakato wa kuandaa Dira mpya na
kushiriki katika kutoa maoni ya kuhusu Tanzania waitakayo miaka ijayo.
Comments