TBA YAANZA KUWAFURUSHA WADAIWA SUGU KWENYE NYUMBA WALIZOPANGA.

TBA YAANZA KUWAFURUSHA WADAIWA SUGU KWENYE NYUMBA WALIZOPANGA.



Na Emmanuel Kawau,

Dar es salaam.

WAKALA wa Majengo Tanzania (TBA) wameanza zoezi la kuwaondoa wadaiwa sugu kwenye nyumba zao walizopanga wakiwemo viongozi na watumishi wa umma ili kupisha wengine wenye uhitaji na watakaolipa kwa wakati bila usumbufu wowote.

Akizungumza na waandishi wa Habari Novemba 29/2023 Kaimu Meneja wa TBA Mkoa wa Dar es Salaam Arch. Bernard Mayemba amesema wameanza kuwaondoa wapangaji wa Nyumba za XNMC zilizopo Mbezi Beach na baadae wanatarajia kuendelea na zoezi katika maeneo mengine ikiwemo Temeke,Masaki na Oster bay ambapo zoezi hilo litadumu kwa muda wa takribani wiki tatu.

Ameongeza kuwa Mkoa wa Dar es Salaam una jumla ya Nyumba 1,200 za Watumishi wa umma na wanagaji wanaodaiwa ni 117 ambapo wanaidaiwa jumla ya Tzs Bilion 1.1, na kila mmoja anadaiwa sio chini ya Tzs milioni moja,mbili na kuendelea.

Mayemba amesema kodi zinazopatikana kwenye nyumba hizo huisaidia TBA kufanya shughuli zake ikiwemo kufanya ukarabati wa nyumba hizo,kuanzisha miradi mipya na kutoa fursa kwa watumishi na watu wengi zaidi kupata nyumba zenye gharama nafuu.

Aidha amebainisha kuwa wadaiwa wote watakaolipa Masaa mawili au mapema zaidi kabla ya kufikiwa na wakala wa mahakama wanaefanyanae kazi yakuwaondoa wadaiwa sugu hawataondolewa kwenye nyumba hizo kwani TBA hupitia mfumo wao na kuangalia waliolipa kabla ya kwenda kuwaondoa masaa mawili kabla ya kuanza zoezi.

"Kuhusu njia za malipo mpangaji anachagua mwenyewe halazimishwi,wapo wasiotaka usumbufu wanaunganisha account zao za mishahara na kulipa moja kwa moja kila mwezi mshahara unapoingia lakini wapo wengi wanalipa wenyewe sasa hawa ndio wenye changamoto"

Pia amesema kuwa ili kupunguza adha hiyo TBA tayari imeshaandaa mfumo maalumu utakaokuwa unampa taarifa mpangaji kiwango anacho daiwa na muda wa kulipa na mfumo huo utakuwa unampiga faini mpangaji ambaye hatalipa kwa wakati kodi yake kila baada ya miezi mitatu.

 

Comments