TCRF IMEIOMBA SERIKALI KUWA NA MIPANGO ENDELEVU KUJENGA UWEZO MIFUMO HAKI WATOTO.

 

Mkurugenzi Mkuu wa Mtandao wa Mashirika ya Haki za watoto ukanda wa Afrika Mashariki na Mataifa zaidi ya Kumi Benedict Omillo akizungumza katika mkutano wa mapendekezo ya wadau kuhusu Haki ya Mtoto katika siku ya Mtoto duniani ambao umeandaliwa na Jukwaa la Haki ya Mtoto Tanzania (TCRF) jijini Dar es salaam.Mratibu wa Kitaifa wa Jukwaa la Haki ya Mtoto Tanzania (TCRF) Ombeni Kimaro akizungumza katika mkutano wa mapendekezo ya wadau kuhusu Haki ya Mtoto katika siku ya Mtoto duniani ambao umeandaliwa na Jukwaa la Haki ya Mtoto Tanzania (TCRF) jijini Dar es salaam.

Mratibu wa Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) Onesmo Olengurumwa akizungumza katika mkutano wa mapendekezo ya wadau kuhusu Haki ya Mtoto katika siku ya Mtoto duniani ambao umeandaliwa na Jukwaa la Haki ya Mtoto Tanzania (TCRF) jijini Dar es salaam.
Mratibu wa Zanzibar Child Right Forum (ZCRF) Sophia Leghela akichangia jamobo mkutano wa mapendekezo ya wadau kuhusu Haki ya Mtoto katika siku ya Mtoto duniani ambao umeandaliwa na Jukwaa la Haki ya Mtoto Tanzania (TCRF) jijini Dar es salaam.Baadhi ya wanafunzi kutoka Shule ya Msingi Bright Hope ambao wamehudhuria katika mkutano huo wa siku ya mtoto Duniani.
Baadhi ya wadau wakitoa maoni yao mkutano wa mapendekezo ya wadau kuhusu Haki ya Mtoto katika siku ya Mtoto duniani ambao umeandaliwa na Jukwaa la Haki ya Mtoto Tanzania (TCRF) jijini Dar es salaam.
 Picha ya Pamoja ya wadau mbalimbalia ambao wameshiriki katika mkutano wa mapendekezo  kuhusu Haki ya Mtoto katika siku ya Mtoto duniani ambao umeandaliwa na Jukwaa la Haki ya Mtoto Tanzania (TCRF) jijini Dar es salaam.

............................

NA MUSSA KHALID

Jukwaa la Haki ya Mtoto Tanzania (TCRF) limeiomba serikali kuwa na Mipango endelevu ya kujenga uwezo kwenye mifumo ya Haki za watoto ikiwemo kuwepo na utaratibu wa Utambuzi wa Maafisa ustawi wa jamii binafsi katika ulinzi wa mtoto.

Akizungumza leo jijini Dar es salaam wakati akiwasilisha mapendekezo ya wadau kuhusu Haki ya Mtoto baada ya kusheherekea siku ya Mtoto duniani,Afisa Program wa Jukwaa Hilo Rogassian Massue amesema kuwa hali za Haki za watoto zinaendelea kupata changamoto kutokana na baadhi ya maeneo watoto kuishi katika Mazingira magumu Kwa kufanyiwa ukatili.

Amesema kuwa mapendekezo ya (TCRF) ni vyema serikali ikashirikiana na  jukwaa la mitandao na wadau katika kutenga rasilimali ya kuweka mikakati yenye viashiria vya usambazi wa sera Kwenye jamii.

"Tukiangalia Haki ya Afya Kwa mtoto Kwa watoto tunaangalia pia Kwa wale watoto ambao hawako Shule Kwa kuishauri serikali pia kuliangalia Hilo katika Mpango wa bima ya Afya Kwa namna watakavyonufaika pia"Amesema Roggasian

Katika Hatua nyingine Jukwaa Hilo limeiomba serikali kuharakisha mchakato wa mabadiliko ya sheria ya ndoa Ili kufanya maamuzi ya kuweza kumsaidia mtoto kutoingia Kwenye ndoa za utotoni.

Awali akizungumza katika Mkutano huo Mkurugenzi Mkuu wa Mtandao wa Mashirika ya Haki za watoto ukanda wa Afrika Mashariki na Mataifa zaidi ya Kumi Benedict Omillo amesema lengo lao ni khakikisha Sauti ya Mtoto inafika maeneo mengi kwani mtoto anahitaji kushirikishwa kikamilifu.

"Amesema kuwa Taasisi hizi za Afrika ya Mashariki sauti ya mtoto itaweza kusikika kwa kikanda na watoto ananafasi Kubwa ya kujieleza Ili tunapounda sera na sheria pia aweze kusikika kikamilifu"amesema Omillo

Mwenyekiti wa Bodi TCRF Godwin Mongi amewataka wadau mbalimbali kutumia fursa hiyo ili kuweza kuboresha maeneo ambayo yatasaidia kuwezeaha Mazingira wezeshi kwa jamii.

Naye Afisa Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria,anayehudumia msaada wa kisheria Laurent Burilo amesema upo umuhimu kwa wadau kuhakikisha watoto waliopo vizuizini wanapata haki zao kwa wakati. 

Baadhi ya watoto wamewashauri wazazi kuwapeleka watoto Shuleni na kupatiwa Haki zao za msingi wanazozihitaji. 

Katika Jukwaa hilo wameshiriki wadau kutoka mashirika mbalimbali likiwemo Shirika la SAVE THE CHILDREN na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu pamoja na maafisa kutoka serikalini.

Comments