TENMET YAPONGEZWA KWA KUANDAA KONGAMANO LA KIMATAIFA LA UBORA WA ELIMU.
TENMET YAPONGEZWA KWA KUANDAA KONGAMANO LA KIMATAIFA LA UBORA WA ELIMU.
Dar es salaam.
Serikali imeahidi Kuendelea kushirikiana sekta binafsi,wadau na Taasisi mbalimbali zinazojihusisha na maswala Elimu katika kuboresha mazingira ya Elimu nchini ili iweze kumkomboa Mtoto wa Kitanzania.
Ahadi hiyo imetolewa leo November 29/2023 na Naibu katibu mkuu wizara ya Elimu DKT. Franklin Rwezimula wakati akifunga Kongamano la Tatu la Kimataifa la Ubora wa Elimu liloandaliwa na Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET) na kuwakutanisha Wadau wa Elimu kutoka Nchi 10 za Afrika.
Dkt Rwezimula amesema kuwa Serikali hajajikita tu katika kutoa ahadi mbalimbali juu ya Elimu bali imeendelea kuboresha mazingira ya Elimu kwa kujenga madarasa na nyumba za walimu,kupitia mitaala,kiboresha sera, Kuboresha uwezo wa walimu kwa kuwapa mafunzo ya mara kwa mara ili kuhakikisha wanakuwa na uwezo wa kuwafundisha wa watoto kulinganana na kasi ya mabadiliko ya Dunia inavyokwenda.
"Serikali itaendelea kuhakikisha elimu nchini inakuwa bora na inayoweza kumkomboa mtoto wa Kitanzania,na ili kufanikisha hilo tutashirikiana na wadau mbalimbali kama TENMET na tunawapongeza kwa kongamano hili ambalo linatoa chachu ya kufanya madiliko mbalimbali katika sekta ya elimu" Amesema Dkt Franklin.
Ameongeza kuwa katika majadiliano yao wameweza kubainisha kuwa kunahitajika kuongeza kasi ya utoaji wa mafunzo mbalimbali ya mara kwa mara kwa walimu ili kuhakikisha elimu wanayowapa wanafunzi inakidhi matakwa ya elimu bora ikiwa ni pamoja na kuwa na mitaala yenye kukidhi matakwa ya Dunia ya sasa na kutoa mawanda mapana ya mtoto kujifunza kidigital na kupewa nafasi ya kuonesha ujuzi na kipawa chake nje ya elimu ya darasani.
Bi Faraja ameongeza kuwa Tenmet kipaumbele chake kikubwa kitaendelea kuwa kuhakikisha Tanzania na Afrika kwa ujumla inakuwa na Elimu bora kulingana na Kasi ya mapinduzi ya nne ya viwanda Dunia.
Comments