RAOMA FOUNDATION YAJA NA KAMPENI YA' TWENZETU DARASANI 2024' KUWAKOMBOA WANAFUNZI NCHINI.

Na Mwandishi wetu T


Na Thadei PrayGod,Dar es salaam.

 Ili kuhakikisha watoto wa kitanzania wanaosihi maisha magumu na kushindwa kumudu mahitaji mbalimbali ya shule ikiwemo kupata sare za shule na madaftari ,Asasi isiyo ya kiserikali ya  Raoma Foundation imezindua kampeni ya Twenzetu darasani 2024 iliyolenga kuhamasisha jamii na wadau kushiriki kuchangia maendeleo ya wanafunzi shuleni.

Akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa Uzinduzi wa kampeni hiyo Mwanzilishi wa Taasisi ya Raoma Foundation, Rahma Mohamed amesema kampeni hiyo inaenda sambamba na  kuiunga mkono Serikali ya awamu ya sita iliyopo chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kukuza elimu na mazingira ya kupata elimu nchini 

Amesema taasisi hiyo  isiyo ya kiserikali inayojiusha na kuiwezesha jamii ipate huduma binafsi za kijamii kupitia mradi huo wamelenga kuwafikia watoto 4509 wenye mahitaji mbalimbali.

''tumeamua kuja na mradi huo ili kuiunga mkono Serikali ya awamu ya sita katika jitihada za kuhakikisha elimu inapatikana bure yenye ubora kwa manufaa ya wananchi wote''alisema Rahma

Hata hivyo aliongeza kuwa kuwa kampeni ya Twenzetu darsani 2024 itaendeshwa Kwa kipindi Cha mwaka mzima  nchi nzima ambapo kwa mikoa ya awali itakayonufaika na mradi huo ni Dodoma, Lindi, Mtwara,Singida, Kigoma pamoja na Akizimkazi Zanzibar.

“Kupitia mradi huu tumelenga kuwafikia watoto 4500 katika Mikoa hii wenye mahitaji kwani mafanikio ya mtoto darasani yanaanza na Mimi na wewe,”amesema Rahma.

Aidha amesema kupitia kampeni hiyo wamelenga kuwapatia watoto mahitaji ya kuanzia nguo zake za shule, madaftari, penseli, madaftari pamoja na kumrekebishia mazingira anayosomea.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Temeke ambaye alikuwa mgeni rasmi katika Uzinduzi wa mradi huo, Sixtus mapunda ameipongeza Taasisi hiyo kuja na mradi huo ambao utawasaidia vijana wanaoishi katika mazingira magumu.

Amesema Serikali inatambua mchango wa Taasisi hiyo kwa kuiunga mkono kwa kutoa fursa ya kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu.

“Kwenye elimu ndo kuna kila kitu kwani imekuwa ikisaidia kumuwezesha mtu kuaminiwa na kumuongezea mtu kujiamini,”amesema.

Balozi wa kampeni hiyo, Tabu Mtingita amesema wamejipanga kupita nyumba kwa nyumba ili kuhakikisha mtoto ambaye amekuwa akishidwa kupata elimu bora anakaa darasani na kupata masomo yake vizuri.

“Kupitia Taasisi ya Rauma Foundation tumejipanga na tutakuwa begabega kufika katika mikoa husika ili kuhakikisha mtoto anasimama na kupata elimu bora,”amesema.

Mkuu wa wilaya ya Temeke Sixtus Mapunda akizungumza katika hafla hiyo ya Uzinduzi
Mwanzilishi wa Taasisi ya Rauma Foundation Rahma Mohamed akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Uzinduzi wa mradi Twezentu darasani 2024 kuzinduliwa

Comments