SEASON 2 YA ZIARA ZA MAKONDA MIKOANI KUANZA TENA

 


 

Na Praygod Thadei

Katibu wa uenezi na itikadi wa chama cha mapinduzi CCM,Paul Makonda leo ametangaza kuanza kwa ziara yake ya msimu wa pili katika mikoa 10 hapa nchini.

Makonda ameyasema hayo jijini Dar es salaam leo wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari juu ya masuala mbalimbali.

Amesema ziara hiyo itaanzia katika mikoa ya Pwani,Tanga,Kilimanjaro,Arusha,Manyara,Singida,Tabora na kuhitimishwa katika wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu.

Amesema katika ziara hiyo ataangazia mambo mbalimbali ikiwemo suala la wananchi kusikilizwa na kufanyiwa kazi changamoto zao katika ofisi za umma kwa kila mkoa atakaotembelea.

''Nawaomba viongozi katika mikoa ambayo nitatembelea wajipange kwani nitasikiliza kero ya kila mwananchi juu ya ofisi za umma kama zinawasikiliza'alisema

Hata hivyo katika hatua nyingine katibu huyo wa itikadi na uenezi amesema wataenda kusheherekea miaka mitatu tangu Rais Dkt Samia aingie madarakani kwa kuwaeleza wananchi mazuri yote yaliyofanywa na serikali.

Ameongeza kuwa serikali imefanya mambo mengi makubwa ikiwemo kukuza sekta za elimu na afya pamoja miundombinu ili wananchi wa Tanzania waishi maisha mazuri.

Comments