DIWANI LYOTO AWAHIMIZA WANANCHI KATA YA MZIMUNI KUPELEKA WATOTO WAO SHULE

DIWANI LYOTO AWAHIMIZA WANANCHI KATA YA MZIMUNI KUPELEKA WATOTO WAO SHULE


            Diwani wa Kata ya Mzimuni Manispaa ya Kinondoni Manfred Lyoto

Na Mussa Augustine.

Diwani wa Kata ya Mzimuni Manispaa ya Kinondoni Manfred Lyoto amewahimiza Wananchi wa Kata hiyo kuwapeleka watoto wao shule pindi shule zitakapofunguliwa Januari 8,2024.

Lyoto ametoa rai hiyo Januari 3 ,2024 Jijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini Kwake ambapo amesema kwamba tayari Serikali imerekebisha Miundombinu Muhimu ya Elimu ikiwemo vyumba vya Madarasa pamoja na Madawati kwa ajili ya wanafunzi wanaoanza kidato cha kwanza na elimu ya Msingi.

"Sisi kama wanamzimuni tumejipanga miundombinu ya shule iko sawa, hivyo naomba wazazi ambao watoto wao wanatakiwa kusajiliwa kwa elimu ya kidato cha kwanza na elimu ya Msingi wahakikishe wanawapeleka watoto wao ili wapate elimu itakayowasaidia katika maisha yao na maendeleo ya Taifa"amesema Lyoto.

Nakuongeza kuwa "Kwenye uongozi wangu suala la elimu ndio kipaumbele changu, kuhamasisha wazazi kupeleka watoto shule hua tunafanya kila mwaka, naomba pia kama kuna wadau wanataka kutoa mchango wao wa madawati au wowote waniite muda wowote nitapokea" amesema.

Kuhusu Utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi amesema kwamba utekelezaji haujafikia asilimia miamoja lakini kwa hatua waliyoitekeleza wanachi wengi wamekua wakipiga simu na kuupongeza uongozi wa kata hiyo kwa kupiga hatua kubwa ya maendeleo katika sekta ya Elimu, Afya,na miundombinu ya barabara.
 
Pia Lyoto amezungumzia kuhusu Ujenzi holela wa majengo ambapo amekiri kwamba ni mapungufu ya upande wa serikali katika kusimamia mipango miji nakwamba zoezi kubadilisha majengo ya zamani ili yawe ya kisasa ambapo mazungumzo na wananchi ,mkandarasi yanaendea ili kufikia adhma hiyo.

" Ujenzi lazima uwe na taratibu za kupata kibali kutoka halmashauri husika kitakachoelekeza suala la mipango miji,hatua ambayo itasaidia kuondokana na ujenzi holela wa makazi jijini hapa"amesema

Katika hatua nyingine amezungumzia kuhusu taasisi ya Mikopo ya "Lyoto Foundation" nakubainisha kwamba taasisi hiyo ameianzisha kwa lengo la kuwasaidia wananchi wa kata ya Mzimuni na wananchi wa maeneo mengine.

" Tumegundua wale wanaokopa hawana elimu ya biashara na  shughuli ya kufanya , mfano mpaka sasa fedha za asilimia kumi za halmashauri shilingi bilioni 5 hazijalipwa , Januari hii tumeruhusiwa kutoa mikopo kupitia taasisi yetu tutahakikisha wale wanaokopa tunawatembelea na kujihakikishia kama wana shughuli za biashara ndio tunawapa mikopo" amesema Lyoto.

 

Comments