HAKUNA HAKI ILIYOVUNJWA UHAMISHO WA WANANCHI,NGORONGORO :NCAA
ka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) imesisitiza kuwa hakuna ukiukwaji wa haki za binadamu katika zoezi la kuwahamisha wananchi wa Ngorongoro kwa hiari na kuwapeleka katika maeneo yaliyotengwa likiwemo la Msomera Wilayani Handeni mkoani Tanga
Hayo yamesemwa mwanzoni mwa wiki mkoani Arusha na Kamishna msaidizi wa uhifadhi ,Mipango ufuatiliaji na Tathmini kutoka Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Lilian Magoma,wakati akizungumza na waandishi wa Habari kwenye ziara ya Waandishi wa habari walipoenda kutazama shughuli za kibinadamu zinazofanyika katika Hifadhi ya Ngorongoro ambazo zinatajwa kuhalibu ustawi wa uhifadhi hiyo.
“Baadhi ya watu toka nje wanatumia vyombo vya habari kusema kunaukiukwaji wa haki za binadamu jambo ambalo sio kweli ,katika utelekezaji wa zoezi hili hakuna jambo ilo kwani tumezingatia sheria na utu katika kuwahamisha”Amesema Magoma.
Magoma,amesema serikali imeingia katika Gharama kubwa ya kuwalipa fidia,kuwasafirisha mali zao na kuwapa motisha ya milioni kumi ambayo ametoa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassani.
Hata hivyo,Magoma ametumia nafasi hiyo kuwataka wananchi wa Ngorongoro kuhama sehemu hiyo kwani kuna faida kubwa ikiwemo kulinda Hifadhi hiyo.
Kwa Upande wake Afisa Uhifadhi Mwandamizi kutoka NCAA,Kassim Nyaki,amesema katika katika awamu hii ya pili iliyoanza mwaka jana lengo ni kujenga nyumba 5000 katika maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya wananchi wa Ngorongoro ikiwemo eneo la Msomela,Kilindi pamoja kitwai mkoani Manyara
Kwamba nyumba hizo 5000 zinatarajiwa kuchukuwa hao.
Nyaki ambaye pia anatoka kwenye Kitengo cha mawasiliano kutoka (NCAA),amesema kwa sasa kila wiki wanahamisha watu na kuwapeleka Msomela.
“Mwamko umeongezeka kwa wananchi kujiandikisha kwa ajili ya kuhama baada ya kuelimishwa na hamasa ni kubwa sana,,changamoto iliyopo ni mwananchi akijiandikisha leo anataka kuhama leo.”Amesema
Nyaki amesema serikali imetoa uhuru kwa wananchi wa Ngorongoro kuchagua sehemu wanayotaka kwenda na sio kuchaguliwa sehemu.
Comments