ACT WÀZALENDO 'YAPULIZA FILIMBI'MBIO ZA UCHAGUZI NDANI YA CHAMA HICHO.

 Mwandishi wetu, Dar 

Chama cha ACT Wazalendo leo kimezindua rasmi zoezi la kuchukua na kurejesha fomu za uongozi ndani ya chama ngazi ya Taifa kwa ajili ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama hicho ambapo zoezi hilo litahitimishwa febuary 24 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam mapema leo hii Mwenyekiti Kamati ya Uchaguzi Taifa, Joran Lwehwbura Bashange amesema kuwa watakao chukua fomu hizo na kurejesha kwa ajili ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ni lazima wawe wamekidhi vigezo ikiwemo kuwa wanachama halali wa chama hicho kwa kulipa ada za uanachama.

Aidha, akitangaza nafasi mbalimbali zinazogombewa ndani ya chama hicho ni pamoja na viongozi wakuu wa kitaifa ambapo ni Kiongozi wa Chama, Mwenyekiti Taifa, Makamu Mwenyekiti Taifa Tanzania Bara pamoja na Makamu Mwenyekiti Taifa Tanzania Zanzibar huku wajumbe wa Halmashauri Kuu ikiwa ni nafasi 24 na ujumbe wa kamati Kuu ni nafasi 24.

"Kwa upande wa Ngome wanawake Taifa, ni nafasi ya Mwenyekiti wa ngome ya wanawake Taifa, Makamu Mwenyekiti, Ujumbe wa Halmashaur Kuu Taifa nafasi 2, Ujumbe Mkutano Mkuu Taifa nafasi 2, huku upande wa Ngome Vijana Taifa ni nafasi ya Mwenyekiti wa ngome ya vijana Taifa, Makamu Mwenyekiti Taifa, Ujumbe halmashauri Kuu Taifa nafasi 2 na Ujumbe wa Mkutano Mkuu nafasi 2" amesema Bashange.

Ameongeza kuwa, utaratibu wa kuchukua fomu na kurejeshwa itakua ni Ofisi ya Makao Makuu ya Chama Magomeni Dar es Salaam, Vuga Zanzibar, Ofisi za mikoa na majimbo yote ya ACT Tanzania nzima huku watakao chukua fomu wakitakiwa kufika na stakabadhi ya malipo ambayo ni bank slip inayoonyesha wamefanya malipo kupitia akaunt ya Chama.

Hata hivyo, ameeleza kuwa wale wagombea wa Ngome ya vijana na wazee wanaporejesha fomu waambatanishe na nyaraka zinazoonesha uthibisho wa umri wao pamoja na picha 2 za passport size wakati wa kurejesha fomu.

Aidha, ameongeza kuwa pamoja na mambo mengine kutakuwa na mdahalo wa watia nia wa uenyekiti Ngome ya vijana feb 20, Uenyekiti  gome Wanawake feb 27 pamoja na wagombea wa nafasi ya kiongozi wa chama na Mwenyekiti wa chama Taifa na Makamu wenyeviti Bara na zanzibar March 4, 2024.

Comments