Skip to main content

BABU OWINO AWAFUNDA VIJANA WA ACT WAZALENDO,AWATAKA KULETA MABADILIKO .

 

 BABU OWINO AWAFUNDA VIJANA WA ACT WAZALENDO,AWATAKA KULETA MABADILIKO .




Mbunge wa Embakassi Mashahidi Nairobi nchini Kenya Dkt. Babu Owino akihutubia Mkutano Mkuu wa Ngome ya Vijana ya Chama Cha ACT Wazalendo.

Na Mwandishi Wetu

MBUNGE wa Jimbo la Embakassi Mashabiki Nairobi nchini Kenya Dkt. Babu Owino amewataka vijana wa chama Cha ACT Wazalendo kupambana katika kuhakikisha nchi inakuwa na maendeleo kwa kuhakikisha wanashiriki kugombea katika chaguzi mbalimbali nchini.

Babu Owino amesema Kama vijana hawatashiriki katika kupigana maendeleo na kushiriki katika chaguzi za viongozi mbalimbali Basi watakuwa hawajalitendea HAKI Taifa kwani wao ni viongozi wa Leo na si kesho Kama wanavyohadaiwa na baadhi ya wanasiasa.

Owino amesema ana imani kubwa kwamba Vijana wa Chama cha ACT Wazalendo wana nguvu ya kuleta mabadiliko chanya na kujenga siku zijazo bora za Tanzania.

 Dkt. Owino amebainisha hayo leo Februari 29, 2024 jijini Dar es Salaam akihutubia Mkutano Mkuu wa ngome ya Vijana wenye lengo la kuchagua Viongozi wa ngome hiyo.

"kijana Kama ukiona hayupo kwenye meza ya chakula ili ule,Basi jua uko kwenye menu Ili uliwe, usikubali pambana na wewe uwe mezani"alisema

“Chama cha ACT Wazalendo kinafahamu kwamba wananchi wa Tanzania walipopigania uhuru walitaka maendeleo na kwamba uhuru wa kila Mtanzania ni haki ya msingi na ndio msingi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” amesema Dkt. Owino.

Ameeleza, ukombozi wa kiuchumi na maendeleo ni nguzo muhimu katika ukombozi halisi wa Afrika, ingawa uhuru wa kisiasa ulikuwa hatua ya kwanza muhimu, bado Tanzania na Afrika zinakabiliwa na changamoto za kiuchumi kama vile umaskini, ukosefu wa ajira, na utegemezi wa nchi zilizoendelea.

Hivyo amesema Chama cha ACT Wazalendo kina dhima ya kutengeneza maisha ya furaha na heshima kwa Watanzania wote kupitia mageuzi ya uchumi ya kutengeneza ajira na huduma bora za kijamii kwa wote.

“Kuendeleza dhamira ya chama na kufanikisha malengo yake kama vijana, tunahitaji nguvu ya umoja. Tunahitaji viongozi wanaoweza kuchukua jukumu muhimu la kuwainua vijana, kuwashirikisha na kuwawezesha,” ameongeza Dkt. Owino.

Kuhusu uchaguzi huo, amewataka kuchagua Viongozi wa waaminifu na waadilifu ambao watatumikia nafasi zao kwa maslahi ya Taifa ikiwemo kupiga vita umasini na ufisadi.

Comments