DUKA JIPYA LA VIATU 'RELAXO' LAFUNGULIWA DAR,MEYA KUMBILAMOTO ATOA KONGOLE KWA MWEKEZAJI
DUKA JIPYA LA VIATU 'RELAXO' LAFUNGULIWA,MEYA KUMBILAMOTO ATOA KONGOLE KWA MWEKEZAJI
Meya Kumbilamoto akikata utepe kuashiria uzimduzi wa duka hilo. |
Na PrayGod Thadei,Dar Es Salaam
Mstahiki meya wa jiji la Dar Es Salaam,Omar Kumbilamoto ameupongeza uongozi wa kampuni ya Best Brand Distributor kwa kuendelea kuwekeza katika maduka ya bidhaa mbalimbali za viatu hapa nchini.
Meya Kumbilamoto ameyasema hayo Leo jijini Dar es salaam wakati akizindua duka jipya (show room) la bidhaa mbalimbali za viatu Relaxo lililopo mtaa wa Morogoro/Samora katikati ya Jiji Hilo,kando ya Barabara ya Mabasi yaendayo haraka (Mwendokasi)
Amesema kuwa uwepo wa duka hilo linalouza viatu vya Relaxo utawafanya wananchi wengi wa Jiji la Dar es salaam hasa wale ambao hawapati muda wa kufanya manunuzi nyakati za mchana kununua bidhaa zao hata nyakati za usiku.
"nawapongeza Sana uongozi wa duka hili chini ya mkurugenzi wake kwa kuendelea kuwekeza kwenye maduka haya ya bidhaa maarufu za viatu na sisi Kama Serikali tunawaunga mkono Kama wawekezaji wazawa" alisema Meya Kumbilamoto.
Aidha ameongeza kuwa na nia ya kampuni hiyo kutaka kuwekeza katika sekta ya viwanda vya bidhaa za viatu hapa nchini kwa kuanza kutengeneza bidhaa hizo hapa hapa nchini ni njema na serikali haitawaacha kwani Jambo Hilo litakuwa msaada kwa serikali kwani itatengeneza ajira mpya kwa watanzania kupitia sekta ya viwanda.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Best Brand Distributor,Khalid M Salim ambaye ni mmiliki wa maduka ya Relaxo amewaambia waandishi wa habari kuwa kampuni hiyo tayari imeshafungua maduka matatu jijini Dar es salaam ikiwemo lililozinduliwa Leo Kati ya maduka 20 inayotegemea kuyafungua mpaka kufikia mwaka 2025 ambayo ni pamoja na duka la Relaxo lililopo Mlimani City,huku la pili likiwa katikati ya Jiji Hilo, mtaa wa Nkurumah eneo la Clock tower.
Amesema maduka hayo (show room) ni mahsusi kwa ajili ya kuuza bidhaa za viatu kutoka chapa (brands) maarufu za viatu duniani za Sparx,Flite,Relaxo na Bahamas zilizosheheni aina mbalimbali za viatu vikieemo vya mazoezi,shule,maabara, hospitali kwa ajili ya madaktari na manesi kwa Mauzo ya jumla na rejareja
"tunatarajia kufungua show room 20 In Shaa Allah Kama hii tuliofungua Leo ili kuwarahisishia wateja wetu kupata huduma zetu pembe zote za Jiji la Dar es salaam na zikifuatiwa pia kufungua nyingine 2 au 3 katika Mikoa yote Tanzania bara na Visiwani"alisisitiza Mkurugenzi huyo wa Best Brand Distributor.
Hata hivyo Bw Khalid ameongeza kuwa tayari kampuni hiyo inayouza viatu kutoka nchi mbalimbali duniani ikiwemo India na Uturuki kupitia maduka yake ya Relaxo imeshaongea na wawekezaji wa utengenezaji wa viatu na wana Mpango wa kuja kuzalisha bidhaa za viatu hapa nchini kwa kuanzisha kiwanda hivyo kuongeza soko la ajira kwa watanzania.
"ndugu waandishi wa habari Kama mnavyoona hapa sisi na wawekezaji ambao ndiyo watengenezaji wa bidhaa za viatu tunazouza katika maduka yetu tuna Mpango pia wa kufungua kiwanda Cha viatu hapa nchini na kuongeza ajira kwa watanzania kwani kupitia maduka yetu haya matatu tayari tumeshatoa ajira kwa zaidi ya watanzania 50" alisema.
Aidha amewaondoa hofu wateja wa maduka yake ya Relaxo yanayouza viatu kutoka chapa za Relaxo,Flite,Bahamas na sparks kwa ajili ya watu wa jinsia zote ikiwemo watoto wa kiume na wa kike kuwa maduka hayo hufunguliwa saa 2 asubuhi na kufungwa saa 2 usiku hivyo wakikosa muda wa kufanya manunuzi asubuhi au mchana wanaweza kufanya manunuzi yao usiku
Kwa upande wao wanafamilia wa kampuni hiyo kupitia Relaxo na Mr Discount Supermarkets ambao Ni watangazaji wa kituo Cha Redio Cha E- fm Cha jijini Dar es,Salim Kikeke na Mpoki wamewashauri watanzania kununua bidhaa za viatu kutoka maduka ya Relaxo kwani ni bidhaa ambazo mtu wa kipato chochote kuanzia Cha chini,Kati na Juu anaweza kuzimudu gharama zake kwani ni rafiki kwa wateja.
- Get link
- X
- Other Apps
Comments