KAMPENI YA UPANDAJI MITI: Kamanda Muliro ataka kupata taarifa za maendeleo ya ukuaji wa miti iliyopadwa kila mwezi.
Na Jeshi la Polisi, Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam SACP. Muliro J. Muliro leo Februari 17, 2024 amezindua kampeni ya upandaji miti katika maeneo yanayomilikiwa na Polisi Jijini Dar es Salaam.
Uzinduzi huo umefanyika katika kambi ya Polisi Kijichi ambapo SACP. Muliro amesema baada ya kupanda miti hiyo ametaka kupata taarifa za maendeleo ya ukuaji wa miti hiyo kila mwezi, kama namna ambavyo kumekuwa na ufuatiliaji wa taarifa za uhalifu.
SACP. Muliro amebainisha kuwa miti hiyo itapandwa katika maeneo mbalimbali yanayomilikiwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam yanayopatikana Kigamboni, Mabwepande na Mwanagati ikihusisha jumla ya miti 3000.
Kampeni hiyo kitaifa ilizinduliwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillus Wambura, Februari 7, 2024 Jijini Dodoma ikiwa na lengo la kupanda miti katika maeneo yanayomilikiwa na Jeshi la Polisi Nchini.
Comments