MCHINJITA AJITOSA,MBIO ZA UCHAGUZI NDANI YA ACT WAZALENDO

 MCHINJITA AJITOSA,MBIO ZA UCHAGUZI NDANI YA ACT WAZALENDO



 Na Mwandishi wetu,

Wakati Chama Cha ACT Wazalendo kikiwa mbioni kuelekea kwenye uchaguzi wake mkubwa wa viongozi mbalimbali unaotarajia kufanyika mapema mwezi ujao,Zoezi la uchukuaji fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya Chama hicho linaendelea kupamba moto ambapo hadi sasa wanachama 25 wamejitokeza kuchukua fomu za nafasi mbalimbali za uongozi huku ikiwa nafasi ya Kiongozi Mkuu wa Chama haijapata mgombea.


Aidha, miongoni mwa nafasi  zilizochukuliwa fomu hizo ni pamoja na nafasi ya   Mwenyekiti Taifa, Makamu Mwenyekiti, Ngome ya Vijana, Wajumbe wa kamati kuu, pamona na Halmshauri Kuu, huku upinzani ukiwa ni mkubwa ndani ya Chama hicho.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Mjumbe wa Kamati ya Uchaguzi Idrissa amesema miongoni mwa wagombea waliojitokeza kugombea nafasi hizo ni pamoja na makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Othman Massoud Othman ambaye anagombea nafasi ya Mwenyekiti Taifa, huku Juma Duni Haji akitetea nafasi yake.


"Zoezi hili lilifunguliwa rasmi Feb 14 ambapo linatarajiwa kufungwa feb 24 mwaka huu, ikiwa leo ni siku ya pili lakini mwitikio umekua mkubwa, ambapo Naibu Waziri Kivuli wa Nishati Isihaka Mchinjita ni miongoni mwa wanachama waliojitokeza kuchukua fomu akigombea nafasi ya Makamo Mwenyekiti Taifa"amesema Idrissa


Akizungumza mbele ya waandishi wa habari mara baada ya kuchukua fomu leo Feb 16, 2024, Isihaka Mchinjita amesema kuwa, miongoni mwa sababu zilizomfanya achukue fomu ya kugombea nafasi hiyo ni pamoja na uwezo wake mkubwa wa kujenga misingi imara ya kitaasisi ndani ya Chama na kupigania ujenzi wa demokrasia pana yenye maslahi ndani ya nchi ya Tanzania.


Aidha amesema kuwa kabla ya kuwa Naibu Waziri Kivuli wa Nishati ndani ya Chama pia aliwai kuwa Mwenyekiti wa Chama Mkoa wa Lindi na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama hivyo amezitumikia nafasi zote kwa uwezo mkubwa na anaamini mchango wake umeacha alama katika kutumikia chama chake.


"Nimezitumikia nafasi zangu zote kwa kadri ya uwezo wangu na imani yangu ni kuwa wanachama wenzangu watakaochukua nafasi hizi wataendelea kuzitumikia katika namna bora zaidi kwa maslahi ya chama chetu na Taifa kwa ujumla"amesema Mchinjita.


Aidha ameongeza kuwa ACT Wazalendo kimepiga hatua kubwa ya ukuaji wake ndani ya muda mfupi ambapo miongoni mwa mambo yaliopiga hatua ni uimarishwaji wa muundo wake jambo ambalo linapaswa kupewa kipaumbele.



Comments