TZLPGA KUENDELEA KUKUZA UELEWEWA,MATUMIZI GESI YA KUPIKIA MAJUMBANI

 



Na PrayGod Thadei

Chama Cha wafanyabiashara wa gesi ya mitungi kwa ajili ya matumizi ya majumbani Tanzania (TZLPGA)kimesema kitaendelea kukuza ushirikiano na wadau mbalimbali ili kukuza matumizi ya gesi ya kupikia hapa nchini (LPG) ili Taifa liwe na matumizi ya nishati hiyo.



Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam na mkurugenzi mtendaji wa chama hicho Amos Jackson Leo February 9,2023 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari na kuongeza kuwa watashirikiana na wadhibiti kupunguza tatizo la ukiukwaji wa Sheria Kama vile ujazaji wa LPG mitaani,usafirishaji wa mitungi ya gesi nje ya nchi bila kibali na wizi wa gesi kutoka kwenye magari makubwa yanayosafirisha.

Ameongeza kuwa chama hicho kilianzishwa mwaka 2023 na wana chama 6 ikiwemo kampuni za Oilcom,O-gas,Lake gas,Manjis gas,Puma gas,Taifa gas na Oryx gas kwa ajili ya kuleta mabadiliko chanya kwenye sekta ya gesi ya kupikia majumbani,kufanya utafiti maalum kwa ajili ya kukusanya takwimu muhimu zinazoweza kusaidia kutengeneza mikakati thabiti katika ukuzaji wa matumizi ya LPG.

Aidha ameongeza kuwa chama hicho pia kitaendelea kushirikiana na taasisi za udhibiti ikiwemo Ewura,Tbs,WMA,Zimamoto ili kuweka na kuboresha viwango katika biashara ya gesi za kupikia majumbani.

Hata hivyo  Bw Jackson amesema kuwa kumekuwa na changamoto kadhaa katika sekta ya gesi ya LPG Ikiwemo ujazaji wa mitungi na watu wahalifu Hali ambayo imepelekea upotevu wa mapato ya serikali.

Naye mkurugenzi wa mamlaka ya udhibiti wa nishati na maji Ewura,Dkt James Andilile amesema uwepo wa chama hicho pia utaisaidia SERIKALI katika azma yake ya kuendeleza matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa wananchi na kuachana na matumizi ya kuni na mkaa.

Dkt Andilile amesema kuwa kwa Mkoa wa Dar es salaam peke yake magunia ya mkaa takribani lako moja hutumika kila mwezi Jambo ambalo linaleta athari kubwa kwa mazingira hivyo wadau wa nishati safi ya kupikia hawana budi kuendeleza kushirikiana na serikali katika kuhamasisha matumizi ya nishati hiyo.

Comments