Skip to main content

ACT WAZALENDO YAAINISHA MAMBO 10 KUONDOA DOSARI UCHAGUZI UJAO WA SERIKALI ZA MITAA

 

ACT WAZALENDO YAAINISHA MAMBO 10 KUONDOA DOSARI UCHAGUZI UJAO WA SERIKALI ZA MITAA


NA MWANDISHI WETU

CHAMA cha ACT Wazalendo kimesisisitiza mambo 10 ili kuhakikisha Uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa una kuwa huru, wa haki na wa kuaminika.

Hayo yameainishwa Naibu Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama hicho Shangwe Ayo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Kwamba pamoja na mambo hayo Amebainisha mambo hayo CHAMA kimetaka Wajumbe wa sasa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Wajiuzulu.

"Kwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameshasaini Sheria mpya ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ya Mwaka 2024 na Sheria hiyo kuchapishwa na Gazeti la Serikali, busara inataka makamishna wote wa Tume ya Uchaguzi Wajiuzulu ili kuwapa Watanzania nafasi ya kupata Tume Mpya ya Uchaguzi," amesema Shangwe na kuongeza,

"Sheria Mpya ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa itungwe kwenye Bunge lijalo.Kama ilivyoainishwa na kifungu cha10 (C)cha Sheria ya Tume Huru ya Uchaguzi, Sheria Mpyaya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa inapaswa kutungwa. ACT Wazalendo tunatoa rai kwa Serikalikuwasilisha Muswada wa Sheria hiyo kwenye kikao kijacho cha Bunge,".

Akitaja mambo hayo 10 ambayo atakwenda kuboresha Sheria Mpya ya Serikali za Mitaa itakayotungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,

Shangwe amesema ni pamoja na karatasi za kupigia kura na nyaraka nyingine za uchaguzi, kwamba Sheria itamke bayana kuwa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi itawashirikisha wadau wa uchaguzi ikiwemo vyam vya siasa katika michakato yote inayohusu karatasi za kupigia kura ili kuepusha kadhia ya karatasi hizo kutumika vibaya kutokana na uzoefu wa Uchaguzi Mkuu 2020 na chaguzi za marudio zilizoitishwa mara sita tangu mwaka 2021.

Jambo lingine amesema ni Uhuru wa Mawakala wa Vyama vya Siasa, kwamba kwa vile wajibu wa mawakala wa vyama vya siasa ni kulinda maslahi yawagombea na vyama vyao, utaratibu wa mawakala kula kiapo cha uaminifu uondoshwe kwneye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

"Wajibu wa kutambulishana kubadilisha mawakala wauchaguzi uachwe kwa vyama vya siasa na wagombea wenyewe. Pia, uhuru wa mawakala kwenye vituo vya kupigia kura uzingatiwe ikiwemo haki ya mawakala kuingia na madaftari ya wapiga kura na simu," ameeleza Shangwe.

Ametaja lingine kuwa ni ulazima wa kubandika matokeo na kugawa nakala za matokeo kwa mawakala, kwamba Sheria iweke sharti kwa wasimamizi wauchaguzi kubandika matokeo katika vituo vya uchaguzi na kugawa nakala ya fomu za matokeo kwa vyama vyote vya siasa

Comments