ACT YAZINDUA SERA YA JINSIA KUTOA FURSA KWA WANAWAKE NDANI NA NJE YA CHAMA HICHO.
ACT YAZINDUA SERA YA JINSIA KUTOA FURSA KWA WANAWAKE NDANI NA NJE YA CHAMA HICHO.
Na mwandishi wetu,
Dar Es Salaam
Akizungumza katika uzinduzi wa sera hiyo ambao umefanyika sambamba na mkutano Mkuu wa ngome ya wanawake wa chama hicho ambao pia utachagua viongozi mbalimbali wa ngome hiyo,Mwenyekiti wa Jukwaa la katiba Tanzania(Jukata) Dkt Ananilea Nkya amekipongeza chama hicho kwa hatua hiyo kubwa Katika siasa za Tanzania.
Dkt Nkya amesema kuzinduliwa kwa sera hiyo ya jinsia kwa chama hicho ni hatua muhimu ambayo itakuwa mfano kwa vyama vingine vya siasa hapa nchini hivyo wanawake wa chama hicho wanapaswa kuisoma na kuifanyia kazi ili kupelekea chama kuzalisha viongozi Bora wanawake.
Hata hivyo Daktari Nkya amekitaka chama Cha ACT Wazalendo kiwekeze katika kuwapika wanawake kuwa majasiri na kupelekea wengi wao kushiriki chaguzi mbalimbali na ngazi za maamuzi ikiwemo uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajia kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.
"Mimi Kama mwalimu na mwanaharakati wa haki za wanawake napenda kuona wanawake wanakuwa viongozi kuanzia ngazi za vijiji na vitongoji mpaka ngazi za juu za Taifa hivyo Kama chama wekezeni rasilimali zenu katika kuwajengea uwezo wanawake"alisema.
Aidha ameongeza kuwa yeye ni miongoni mwa watu ambao hawapendi uwepo wa viti maalum bungeni maana vinawapumbaza baadhi ya wanawake kuona Kama viti hivyo ni Kama huruma kwao hivyo Kama havitakuwepo na kuwekwa Sheria ya usawa wa kijinsia yaani 50 kwa 50 basi wanawake wengi watagombea majimboni na baadaye kushika hatamu za uongozi bungeni bila kupendelewa kutokana na jinsia zao.
Ameongeza rasilimali za chama Cha ACT Wazalendo ni muhimu kuwekeza kwa wanawake kwani wanaweza na uzinduzi wa sera ya wanawake ni daraja muhimu na kipimo Cha kukipa nguvu chama hicho katika siasa za Tanzania na Dunia kwa ujumla.
Awali akizungumza katika uzinduzi wa sera hiyo ulioenda sambamba na uchaguzi wa viongozi wa ngome ya wanawake Taifa,Makamo mwenyekiti wa ACT Wazalendo,Bara Bi Dorothy Semu amesema kuwa sera hiyo ilipitishwa na Halmashauri kuu ya Chama kwa kutambua Bado Kuna ombwe kubwa la wanawake kushiriki siasa na kwenye ngazi za maamuzi,
Hivyo kupitia sera hiyo ya jinsia Sasa wanawake wa chama hicho watapata fursa za kushika hatamu za uongozi ndani na nje ya chama.
Amesema sera hiyo ndiyo sera pekee ya chama Cha siasa hapa nchini kuwatambua na kuwathamini wanawake kwa kuwawekea taratibu zitakazowafanya kushiriki siasa na ngazi za maamuzi ambapo itahakikisha katika nafasi za viongozi wakuu wa kitaifa wa chama,angalau asilimia 30 wanakuwa ni wanawake.
Naye mkurugenzi wa shirika la Wildaf ambao Ni moja ya wawezeshaji waliofanikisha kupatikana kwa sera hiyo,Bi Anna Kulaya amekishukuru chama hicho kwa kutoa ushirikiano kwao na kuongeza kuwa kupitia sera hiyo ya jinsia Sasa wanawake watapata fursa zaidi ndani ya chama ikiwa sera hiyo ni takwa la kisheria katika Sheria ya vyama vya siasa.




Comments