Skip to main content

AKIBA COMMERCIAL BANK YAFUTURISHA WATEJA, WAFANYAKAZI NA WADAU

 

AKIBA COMMERCIAL BANK YAFUTURISHA WATEJA, WAFANYAKAZI NA WADAU





Habari mbalimbali katika picha kwenye hafla ya futari iliyoandaliwa na Akiba Commercial Bank jijini Dar es Salaam.

NA MWANDISHI WETU

Akiba Commercial Bank (ACB) imewafuturisha wateja, wafanyakazi na wadau mbalimbali wa Benki hiyo.

Akizungumza katika hafla hiyo ya futari iliyofanyika Machi 25, 2024 jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa ACB Silvest Arumasi alitumia fursa hiyo kuwapongeza Waislamu wote kwa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

Arumasi amewashukuru wadau wote kwa kutenga muda wao na kujumuika pamoja katika Futari hiyo kwani kitendo hicho kimeleta faraja na heshima kubwa sana.

Aidha, alisema kuwa, ACB imekuwa na utamaduni wa kufanya hafla ya kufuturisha kila mwaka kwa ajili ya kuunga mkono Waislam katika funga yao na pia ni njia nzuri ya kuboresha mahusiano ya benki na wateja wake.

"Akiba Commercial Bank inatambua na kuheshimu sana Imani za wateja, Wafanyakazi na wadau wake na kuupa umuhimu wa kipekee katika mwezi Mtukufu wa Ramadhan," alisema Arumasi.

Arumasi alisema kuwa ACB inaendelea kuboresha na kupanua wigo wa huduma zake ili kuendana na soko kwa lengo ya kukidhi matarajio ya wateja.

Alitumia fursa hiyo kuwaomba wateja na umma kwa ujumla kuendelea kuiamini Benki hiyo ambayo imeweza kuwahudumia Watanzania wengi na kuleta maendeleo makubwa kwa wajasiriamali na Jamii nzima kwa ujumla.

Akiba Commercial BankBenki kwa maendeleo yako.

Comments